Nzi-vunjajungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nzi-vunjajungu
Pseudoclimaciella sp.
Pseudoclimaciella sp.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Neuroptera (Wadudu walio na mabawa wenye vena nyingi kama kimia)
Linnaeus, 1758
Nusuoda: Hemerobiiformia
Familia ya juu: Mantispoidea
Familia: Mantispidae
Leach, 1815
Ngazi za chini

Nusufamilia 4:

Nzi-vunjajungu ni wadudu wadogo kiasi wa familia Mantispidae katika oda Neuroptera (wadudu mabawa-vena) ambao wana miguu ya mbele inayofanana na ile ya vivunjajungu.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Nzi-vunjajungu wana urefu wa kati ya mm 5 na 47 na wana upana wa mabawa wa mm 5-30. Kadhaa, kama spishi za Pseudoclimaciella, huiga nyigu, lakini wengi sana ni hudhurungi pamoja na rangi za kijani, njano na pengine nyekundu. Majina ya kienyeji na ya kisayansi yametokana na muonekano wao wa vivunjajungu, kwani miguu yao ya mbele yenye miiba imetoholewa ili kukamata mawindo ya wadudu wadogo na inafanana sana na miguu ya mbele ya vivunjajungu (tofauti pekee ni kwamba vibano hukosa nyayo na havitumiwi kutembea kabisa). Wana mabawa manne kama viwambo ambayo yanaweza kuwa na ruwaza pengine (haswa katika spishi zinazoiga nyigu) lakini kwa kawaida huwa mangavu.

Wapevu ni wadudu mbuai ambao hukiakia usiku mara nyingi na huvutiwa pengine na taa. Hujilisha kwa wadudu wenye ukubwa unaofaa, ambao huwakamata kama vile vivunjajungu. Walakini, mifumo ya msingi ya mwenendo wa kukamata mawindo ni tofauti kati ya nzi-vunjajungu na vivunjajungu. Nzi-vunjajungu ni wawindaji wamilifu, lakini kama ilivyo na Neuroptera wengine, huruka kwa ugumu.

Lava wa Symphrasinae ni vidusia vya kukaa juu ya lava wa nyuki, nyigu au bungo-mavi. Lava wa Calomantispinae ni mbuai wa arithropodi wadogo, mara nyingi lava wao. Mantispinae wana maendeleo maalumu zaidi ya lava kati ya nzi-vunjajungu wote wanaochunguliwa hadi leo (historia ya maisha ya Drepanicinae bado haijulikani): lava wao hutafuta buibui wa kike au vifuko vyao vya mayai ambayo huingia kujilisha kwa mayai. Lava wa hatua ya kwanza wa mantispinae wanafanana na wadudu mikia-miwili (campodeiform: umbo la Campodea). Wanatumia mikakati miwili kupata mayai ya buibui: wanaweza kupenya moja kwa moja hariri ya vifuko vya mayai wanavyopata, au wanaweza kupanda na kubebwa na buibui wa kike kabla ya uzalishaji wa kifuko (phoresy) na huingia kwenye kifuko wakati kinapojengwa. Lava wanaopanda buibui huchukua nafasi kwenye au karibu na pediseli kwa kawaida; spishi fulani zinaweza kuingia kwenye mapafu-kitabu ya buibui. Wanajitunza juu ya buibui kwa kujilisha kwa hemolimfi yake. Uhamisho wa lava kutoka buibui hadi buibui unawezekana wakati wa kupandana au wa ulaji wa wenzao. Vikundi vikuu vyote vya buibui wawindao vinashambuliwa na nzi-vunjajungu wanaopanda buibui. Vifuko vya mayai vya spishi zinazojenga tandabui pia huingizwa na wapenyaji wa vifuko vya mayai. Ndani ya kifuko cha mayai lava hubambua kuwa na umbo linalofanana na mabuu ya bungo-mavi (scarabaeiform). Kisha huanza kujilisha kwa mayai wakitoa yaliyomo ndani yao kupitia mrija wa kutoboa/kufyonza ulioundwa kwa mandibula na maksila zilizotoholewa. Hatua ya mwisho inageuka kuwa bundo.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

  • Afromantispa capeneri
  • Afromantispa dispersa
  • Afromantispa incorrupta
  • Afromantispa meadewaldina
  • Afromantispa moucheti (Tanzania)
  • Afromantispa nana
  • Afromantispa nanyukina (Kenya)
  • Afromantispa natalensis
  • Afromantispa navasi (Tanzania)
  • Afromantispa tenella (Kenya, Tanzania)
  • Afromantispa verrucutula (Kenya, Uganda)
  • Afromantispa zonaria (Tanzania)
  • Afromantispa zonata
  • Cercomantispa condei
  • Cercomantispa decellei
  • Cercomantispa finoti
  • Cercomantispa keiseri
  • Cercomantispa mozambica
  • Cercomantispa natalica
  • Cercomantispa ndjallai
  • Cercomantispa nigricornis
  • Cercomantispa paolina
  • Cercomantispa perparva (Tanzania)
  • Cercomantispa picea
  • Cercomantispa pulla
  • Cercomantispa stenostigma
  • Cercomantispa tristella
  • Cercomantispa tristis (Uganda)
  • Cercomantispa vulpes (Tanzania, Uganda)
  • Madantispa minuta
  • Madantispa pauliani
  • Madantispa seyrigi
  • Mantispa basilei
  • Mantispa castaneipennis
  • Mantispa centenaria
  • Mantispa delicata
  • Mantispa ellenbergeri
  • Mantispa elpidica
  • Mantispa finoti
  • Mantispa flavinota
  • Mantispa fuliginosa
  • Mantispa fuscipennis (Tanzania)
  • Mantispa guttula
  • Mantispa haematina
  • Mantispa haugi
  • Mantispa loveni (East Africa)
  • Mantispa lutea
  • Mantispa marshalli
  • Mantispa negusa
  • Mantispa phaeonota
  • Mantispa pygmaea (Tanzania)
  • Mantispa tessmanni
  • Nampista africana
  • Nampista auriventris
  • Nampista ragazziana
  • Necyla flavonotata (Uganda)
  • Necyla pupa
  • Paulianella neocopina
  • Paulianella olsufievi
  • Pseudoclimaciella alberti
  • Pseudoclimaciella apicipennis (Kenya, Ruanda, Tanzania)
  • Pseudoclimaciella cachani
  • Pseudoclimaciella congensis
  • Pseudoclimaciella coronata (Uganda)
  • Pseudoclimaciella elisabethae (Uganda)
  • Pseudoclimaciella erichsonii
  • Pseudoclimaciella flava
  • Pseudoclimaciella ivoiriensis
  • Pseudoclimaciella loanga (Kenya, Tanzania)
  • Pseudoclimaciella rubida (Tanzania)
  • Pseudoclimaciella sanguinea
  • Pseudoclimaciella sarta
  • Pseudoclimaciella stitzi (Tanzania)
  • Pseudoclimaciella timmerhansi
  • Pseudoclimaciella thomensis
  • Pseudoclimaciella trivenata
  • Pseudoclimaciella tropica
  • Pseudoclimaciella umbripennis
  • Rectinerva braconidiformis
  • Sagittalata austroafrica
  • Sagittalata bequaerti (Tanzania)
  • Sagittalata bitschi
  • Sagittalata delamarei
  • Sagittalata dorsalis
  • Sagittalata girardi
  • Sagittalata griveaudi
  • Sagittalata hilaris (Uganda)
  • Sagittalata jucunda
  • Sagittalata lugubris
  • Sagittalata nubila
  • Sagittalata pusilla (Uganda)
  • Sagittalata semeriai
  • Sagittalata similata
  • Sagittalata royi
  • Sagittalata tincta
  • Sagittalata vassei

Jenasi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

  • Allomantispa
  • Anchieta
  • Asperala
  • Austroclimaciella
  • Austromantispa
  • Buyda
  • Calomantispa
  • Campanacella
  • Campion
  • Climaciella
  • Dicromantispa
  • Ditaxis
  • Drepanicus
  • Entanoneura
  • Euclimacia
  • Eumantispa
  • Gerstaeckerella
  • Haematomantispa
  • Leptomantispa
  • Mimetispa
  • Nolima
  • Orientispa
  • Paramantispa
  • Plega
  • Spaminta
  • Stenomantispa
  • Theristria
  • Toolida
  • Trichoscelia
  • Tuberonotha
  • Xaviera
  • Xeromantispa
  • Zeugomantispa

Picha[hariri | hariri chanzo]