Nyumba ya Haki ya Ulimwengu
Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ni asasi yenye wajumbe tisa ambayo ina mamlaka ya juu kabisa katika Dini ya Kibaháʼí. Iliundwa na Baháʼu'lláh, mwanzilishi wa Dini ya Kibaháʼí, kama asasi ambayo inaweza kutunga sheria juu ya masuala ambayo hayajashughulikiwa waziwazi katika maandiko matakatifu ya Bahá'u'lláh, ikitoa nafasi kwa Dini ya Kibaháʼí kuendana na mabadiliko ya hali.[1] Uchaguzi wake wa kwanza ulifanyika mwaka 1963, na kisha kila baada ya miaka mitano, na wajumbe walichaguliwa na wajumbe wa Mabaraza ya Kiroho ya Kitaifa ya Wabaháʼí kutoka kote duniani.
Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, kama kiongozi wa dini hii, imekuwa ikitoa mwongozo kwa jumuiya ya Wabaháʼí ulimwenguni kote hasa kupitia mipango ya miaka kadhaa, pamoja na ujumbe wa kila mwaka unaotolewa wakati wa sherehe ya Ridván. Ujumbe huo umelenga katika kuongeza idadi ya Mabaraza ya Kiroho ya Mahali, kutafsiri fasihi za Kibaháʼí, kuanzisha Vituo vya Wabaháʼí, kukamilisha Nyumba za Ibada za Kibaháʼí, kufanya mikutano ya kimataifa, na kuendeleza mifumo ya elimu ili kuboresha kusoma na kuandika, jukumu la wanawake, hali za kiroho za watoto na vijana, maisha ya kifamilia, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na ibada ya pamoja.[2] Nyumba ya Haki ya Ulimwengu pia imekuwa na jukumu katika kukabiliana na mateso ya kimfumo ya Wabaháʼí nchini Iran kwa kuvutia umakini wa vyombo vya habari duniani kote.[3]
Vitabu na nyaraka zilizochapishwa na Nyumba ya Haki ya Ulimwengu zinachukuliwa kuwa vya mamlaka na maamuzi yake yanachukuliwa kuwa yasiyoweza kukosewa na Wabahá'í.[4] Ingawa ina mamlaka ya kutunga sheria katika mambo ambayo hayajashughulikiwa kwenye maandiko matakatifu ya Kibaha'i, Nyumba ya Haki ya Ulimwengu mara chache imefanya kazi hii.[5]
Makao ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu na wajumbe wake wanaishi huko Haifa, Israeli, kwenye mteremko wa Mlima Karmeli.[1] Uchaguzi wa hivi karibuni zaidi ulikuwa tarehe 29 Aprili 2023.[6] Ingawa nafasi zote nyingine za kuchaguliwa na kuteuliwa katika Dini ya Kibaháʼí ziko wazi kwa wanaume na wanawake, ujumbe katika Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ni kwa wanaume pekee; maandiko ya Kibaháʼí yanaonesha kwamba sababu ya hili itakuwa wazi katika siku zijazo.[7]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Bahá'u'lláh, mwanzilishi wa Dini ya Kibaha'i, katika kitabu chake Kitáb-i-Aqdas [Kitabu Kitakatifu Kabisa] kwanza anaagiza kuundwa kwa asasi ya Nyumba ya Haki na kufafanua majukumu yake. Majukumu ya asasi hii pia yamefafanuliwa na kurejelewa katika maandiko mengine kadhaa ya Bahá'u'lláh ikiwemo katika Nyaraka zake zilizofunuliwa baada ya Kitab-i-Aqdas. Katika maandiko hayo Bahá'u'lláh anaandika kuwa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu itachukua mamlaka juu ya dini hiyo, na kufikiria masuala ambayo hayakuwa yametajwa na yeye mwenyewe; alisema kuwa wajumbe wa asasi hiyo watahakikishiwa msukumo wa kimungu, na watajali watu wote na kulinda utu wao[1]
Baadaye, ʻAbdu'l-Bahá, mwana wa Baháʼu'lláh na mrithi wake, katika Wosia na Agano lake, alifafanua kuhusu utendaji wake, muundo wake na akaelezea njia ya uchaguzi wake. Aliandika kwamba Nyumba ya Haki ya Ulimwengu itakuwa chini ya ulinzi, hifadhi na mwongozo usio na dosari wa Baháʼu'lláh, kwamba itakuwa huru kutokana na makosa, na kwamba utiifu kwake utakuwa ni wa lazima. ʻAbdu'l-Bahá alikuwa wa kwanza kutumia jina la "Nyumba ya Haki ya Ulimwengu" ili kutofautisha chombo cha juu zaidi kutoka kwa 'Nyumba za Haki' za kawaida zitakazoanzishwa katika kila jamii, na 'Nyumba za Haki' za kati (ambazo ni mabaraza ya kiroho ya kitaifa ya Wabaháʼí kwa sasa). Pia alisema kwamba maamuzi ya chombo hicho yanaweza kufanywa kwa kura ya wingi, lakini maamuzi yanayoungwa mkono na wote yalikuwa ni bora zaidi, na kwamba ingechaguliwa na wajumbe wa Nyumba za Haki za kati. Pia alithibitisha maneno ya Baháʼu'lláh kwamba ingawa wanawake na wanaume ni sawa kiroho, ujumbe katika Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ungekuwa tu ni kwa wanaume, na kwamba hekima ya uamuzi huu ingekuwa wazi siku zijazo (ona Baháʼí Faith and gender equality).[1]
Wakati wote ʻAbdu'l-Bahá na Shoghi Effendi, viongozi wa dini baada ya Baháʼu'lláh, walifikiria kuanzisha Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, wote wawili walikataa kufanya hivyo. Sababu ya Shoghi Effendi ilikuwa imani yake katika udhaifu wa asasi za Kibaháʼí zilizokuwepo — kulikuwa na idadi ndogo sana ya mabaraza ya kiroho ya kitaifa na mabaraza ya kiroho ya mahali. Hivyo basi, wakati wa uhai wake, Shoghi Effendi alijiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, kwa kuanzisha muundo wa kiutawala imara katika ngazi ya mahali na kitaifa. Mnamo mwaka wa 1951 kulipokuwa na Mabaraza 9 ya Kiroho ya Kitaifa, Shoghi Effendi aliteua wajumbe wa Halmashauri ya Kimataifa ya Wabaháʼí, na akaielezea kama maandalizi ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ambayo ingefuata. Baada ya kifo cha ghafla cha Shoghi Effendi mwaka wa 1957, Mikono wa Hoja waliongoza mambo ya dini na kutangaza kwamba uchaguzi wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ungefanyika mwaka wa 1963 mwishoni mwa Mpango wa Miaka Kumi, mpango wa ufundishaji wa kimataifa uliowekwa na Shoghi Effendi.[1]
Mnamo mwaka wa 1961, Halmashauri ya Kimataifa ya Wabaháʼí ilibadilishwa kuwa chombo kilichochaguliwa, na wajumbe wa Mabaraza yote ya Kiroho ya Kitaifa walipiga kura kuchagua wajumbe wake. Kisha mnamo Aprili 1963, Nyumba ya Haki ya Ulimwenguni ya kwanza ilichaguliwa, miaka sita baada ya kifo cha Shoghi Effendi, na Mabaraza 56 ya Kiroho ya Kitaifa. Tarehe ya uchaguzi huo ililingana na kukamilika kwa Harakati za Mpango wa Miaka Kumi na pia na maadhimisho ya miaka mia moja ya tangazo la hadharani la Baháʼu'lláh katika Bustani ya Ridván mnamo Aprili 1863. Tangu wakati huo, Nyumba ya Haki ya Ulimwenguni imekuwa ikifanya kazi kama kiongozi wa dini – wajumbe binafsi hawana mamlaka, ni kama mkusanyiko tu ndiyo wanayo mamlaka. Mnamo 1972 ilichapisha katiba yake.[1][8]
Mchakato wa Uchaguzi
[hariri | hariri chanzo]Nyumba ya Haki ya Ulimwengu huchaguliwa kupitia kura ya siri na kura ya wingi katika uchaguzi wa hatua tatu na Wabaháʼí watu wazima ulimwenguni kote. Nyumba ya Haki huchaguliwa bila uteuzi au kampeni na wanaume watu wazima wa dini ya Kibaháʼí wanastahiki kuchaguliwa kuwa wajumbe wa Nyumba.[9] Chombo hiki huchaguliwa kila baada ya miaka mitano na wajumbe wa Mabaraza mbalimbali ya Kiroho ya Kitaifa (NSA) kote duniani. Kila mjumbe wa Mabaraza ya Kiroho ya Kitaifa mbalimbali, ambao wenyewe walichaguliwa na Wabaháʼí wa nchi yao, hupiga kura kuchagua Wabaháʼí wanaume watu wazima tisa. Wale wasiokuwepo kufika kwenye mkusanyiko wa uchaguzi huweza kutuma kura zao au kubebwa na wawakilishi ambao wataweza kushiriki. Watu tisa ambao wanapata kura nyingi zaidi huchaguliwa kuwa wajumbe wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu.
Mnamo mwaka wa 2013, ukijumuisha kura za walioweza kufika Haifa, na zile za wale ambao hawakuweza kufika ambazo zilikuwa ni kura 400, jumla ya kura ilikuwa ni zaidi ya 1500.[10] Uchaguzi huu uliadhimisha miaka 50 tangu uchaguzi wa kwanza wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu mwaka 1963.[11][12]
Uchaguzi kamili wa hivi karibuni ulikuwa tarehe 29 Aprili 2023.[13][14]
Majukumu
[hariri | hariri chanzo]
Nyumba ya Haki ya Ulimwengu leo inaongoza ukuaji na maendeleo ya jamii ya Wabaha'i duniani. Majukumu ya jumla ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, kama yalivyotajwa na Baháʼu'lláh, ni pamoja na kukuza Hoja ya Mungu, kuhifadhi sheria, kusimamia mambo ya kijamii, kuelimisha nafsi za watu, kuhakikisha elimu ya watoto, kufanya dunia nzima istawi (kuondoa tofauti za kuwa na mali nyingi na umasikini uliopitiliza), na kuwajali wazee na wagonjwa ambao wako katika umaskini.[15] Kulingana na katiba ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, baadhi ya uwezo na majukumu yake ni pamoja na:[15]
- Kukuza sifa za kiroho zinazowatambulisha Wabaha'i binafsi na kwa pamoja
- Kuhifadhi, kutafsiri na kuchapisha maandiko matakatifu ya Kibaháʼí
- Kulinda na kutetea jamii ya Wabaha'i duniani kutokana na udhalimu na mateso
- Kuhifadhi na kukuza Kituo cha Kiroho na Kiutawala cha Imani ya Kibaháʼí duniani
- Kuhamasisha ukuaji na ukomavu wa jamii ya Wabaha'i na utawala
- Kulinda haki za kibinafsi, uhuru na ubunifu wa mtu binafsi
- Kutumia kanuni na sheria za Kibaháʼí
- Kuendeleza, kufuta na kubadili sheria ambazo hazijaandikwa katika maandiko matakatifu ya Kibaháʼí, kulingana na mahitaji ya wakati
- Kutoa vikwazo dhidi ya uvunjaji wa sheria za Kibaháʼí
- Kutatua na kusuluhisha mizozo iliyowasilishwa kwake
- Kusimamia fedha zote za kidini na malipo kama Huqúqu'lláh zilizokabidhiwa kwake.
Zaidi ya hayo, Nyumba ya Haki ya Ulimwengu imeagizwa na Baháʼu'lláh kutumia ushawishi chanya kwa ustawi wa jumla wa wanadamu, kuendeleza amani ya kudumu kati ya mataifa ya dunia, kuhakikisha "mafunzo ya watu, ujenzi wa mataifa, ulinzi wa mwanadamu na kuhifadhi heshima yake".[15][16]
Mamlaka
[hariri | hariri chanzo]Nyumba ya Haki ya Ulimwengu pia imepewa jukumu la kunyumbulisha Dini ya Kibaháʼí kadiri jamii inavyoendelea, na hivyo imepewa uwezo wa kutunga sheria kuhusu masuala ambayo hayajawekwa wazi katika maandiko matakatifu ya Kibaháʼí. Ingawa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ina mamlaka ya kubadili au kufuta sheria zake yenyewe inapoendana na mabadiliko ya hali, haiwezi kufuta au kubadilisha sheria yoyote iliyoandikwa wazi katika maandiko matakatifu.[1][15]
Machapisho
[hariri | hariri chanzo]Wakati Nyumba ya Haki ya Ulimwengu imepewa uwezo wa kutunga sheria juu ya mambo mbalimbali, limekuwa likitumia mamlaka haya kwa kiwango kidogo tangu kuanzishwa kwake mnamo 1963. Badala yake, limekuwa likitoa mwongozo wa jumla kwa Wabahá’í ulimwenguni kote, na si sheria maalum; mwongozo huu kwa ujumla umekuwa katika mfumo wa barua na ujumbe, kama mawasiliano ya Shoghi Effendi. Barua nyingi kati ya hizi zimechapishwa katika makusanyo na zinachukuliwa kuwa zina nguvu za kiungu na mamlaka; maamuzi yake yanachukuliwa kuwa yasiyoweza kukosewa na Wabahá’í.[17][4] Barua hizo zinashughulikia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufundishaji, sala, maisha ya familia, elimu na utawala wa Kibahá'í.[17] Kila mwaka siku ya kwanza ya Ridván (ambayo inaweza kuwa Aprili 20 au 21 kulingana na tarehe ya Naw-Rúz), Nyumba ya Haki ya Ulimwengu hutuma ujumbe kwa jamii ya Wabahá’í ulimwenguni pote, unaojulikana kama ujumbe wa Ridván.[18]
Asasi hii pia imekusanya na kuchapisha dondoo kutoka kwa maandiko ya Báb, Baháʼu'lláh na ʻAbdu'l-Bahá. Mnamo 1992 walichapisha Kitáb-i-Aqdas, kitabu cha sheria za Baháʼu'lláh kwa Kiingereza, na tafsiri zaidi zimechapishwa tangu wakati huo.[17] Katika juhudi hizi, walianzisha idara za utafiti na kumbukumbu katika Kituo cha Wabaháʼí cha Ulimwengu, na, hadi mwaka wa 1983, wamekusanya zaidi ya barua 60,000 za Baháʼu'lláh, ʻAbdu'l-Bahá na Shoghi Effendi. Kazi hizi zilizokusanywa zimetumiwa kama msingi katika mashauriano ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu.[17]
- Ahadi ya Amani ya Ulimwenguni (1985) [19]
- Tamko lililowekwa "Kwa Watu wa Ulimwengu", lililowasilishwa kwa zaidi ya viongozi 160 wa serikali. Inabainisha mahitaji makuu ya, na pia vikwazo vinavyopinga, kuanzishwa kwa amani ya ulimwengu.
- Baháʼu'lláh (1992)
- Kukumbuka miaka mia ya kifo cha Baháʼu'lláh, taarifa hii ni muhtasari wa maisha na kazi zake.
- Ufanisi wa Wanadamu (1995)
- Maelezo juu ya dhana ya ustawi wa ulimwengu katika muktadha wa Mafundisho ya Kibaháʼí.
- Karne ya Mwanga (2001)
- Muhtasari wa karne ya 20, ukiangazia mabadiliko makubwa na kuibuka kwa Dini ya Kibaha'i kutoka kwenye kutojulikana.
- Barua inayozungumzia tatizo la chuki za kidini. Inatoa wito kwa harakati zote za kidini "kuondokana na taratibu zisizobadilika zilizorithiwa kutoka zamani ziliyopita."
- Imani Moja ya Kawaida (2005)
- Waraka uliokusudiwa hasa kwa hadhira ya Wabaháʼí, ambao unatambua jukumu kuu kwa jamii ya Wabaháʼí ni kupanda kanuni ya umoja wa dini na kushinda ubaguzi wa kidini.
Wajumbe wa sasa
[hariri | hariri chanzo]Wajumbe wote wa sasa wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ni:[20]
- Paul Lample (2005)
- Payman Mohajer (2005)
- Shahriar Razavi (2008)
- Ayman Rouhani (2013)
- Chuungu Malitonga (2013)
- Juan Francisco Mora (2018)
- Praveen Mallik (2018)
- Albert Nshisu Nsunga (2023)
- Andrej Donoval (2023)
Wajumbe wa Zamani
[hariri | hariri chanzo]Matokeo ya uchaguzi wa awali wa mwaka 1963 ulikuwa ni wajumbe watano kutoka Halmashauri ya Kimataifa ya Wabaháʼí, wawili kutoka Baraza la Kiroho la Kitaifa (NSA) la Marekani, mmoja kutoka NSA ya Uingereza, na mmoja kutoka NSA ya India.[21]
Wajumbe wameingizwa kwenye jedwali chini ya mwaka walipochaguliwa kwa mara ya kwanza. Kuanzia na uchaguzi wa kwanza mwaka 1963, uchaguzi wa kawaida wa wanachama wote hufanyika kila baada ya miaka mitano, na kumekuwa na chaguzi ndogo mara tano, zilizoonyeshwa kwenye jedwali kwa italiki, mnamo 1982, 1987, 2000, 2005 na 2010. Wajumbe wote wameendelea kuhudumu baada ya kuchaguliwa tena katika chaguzi zilizofuata. Amoz Gibson, Charles Wolcott, na Adib Taherzadeh walifariki wakiwa ofisini wakati walipokuwa wajumbe, wengine waliruhusiwa kustaafu.
1963 | 1968 | 1973 | 1978 | 1982 | 1983 | 1987 | 1988 | 1993 | 1998 | 2000 | 2003 | 2005 | 2008 | 2010 | 2013 | 2018 | 2023 |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Lutfu'lláh Hakím | David Ruhe | Farzam Arbab* | Ayman Rouhani | ||||||||||||||
Amoz Gibson | Glenford Mitchell | Gustavo Correa | Praveen Mallik | ||||||||||||||
Charles Wolcott | Peter Khan | Stephen Hall | Andrej Donoval | ||||||||||||||
David Hofman | Hooper Dunbar | Stephen Birkland | Albert Nshisu Nsunga | ||||||||||||||
Borrah Kavelin | Adib Taherzadeh | Kiser Barnes | Chuungu Malitonga | ||||||||||||||
Hugh Chance | J. Douglas Martin[22][23] | Paul Lample | |||||||||||||||
Ali Nakhjavani | Hartmut Grossmann | Shahriar Razavi | |||||||||||||||
Hushmand Fatheazam | Firaydoun Javaheri | Juan Francisco Mora | |||||||||||||||
Ian Semple | Payman Mohajer |
- Farzam Arbab (Oktoba 27, 1941 – Septemba 25, 2020), alizaliwa Tehran, Iran alikuwa mwanachama kutoka 1993 hadi alipoachia ujumbe wake mwaka 2013, akiwa na umri wa miaka 71.[24][25]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 Smith 2000, pp. 346–350.
- ↑ Smith 2000, p. 348.
- ↑ Javaheri, Firaydoun (Desemba 2018). "Ustahimilivu Mzuri". The Journal of Bahá'í Studies. 28 (4). Association for Bahá'í Studies: 7–22. doi:10.31581/jbs-28.4.2(2018). ISSN 0838-0430. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Januari 5, 2023. Iliwekwa mnamo Jan 5, 2023.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 The World of the Bahá'í Faith… The Universal House of Justice 2022.
- ↑ Khan, Peter J. (Des 1999). "Some Aspects of Bahá'í Scholarship". The Journal of Bahá'í Studies. 9 (4). Association for Bahá'í Studies: 51. doi:10.31581/jbs-9.4.3(1999). ISSN 0838-0430. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Januari 5, 2023. Iliwekwa mnamo Jan 5, 2023.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Baháʼí International Community 2018.
- ↑ Smith 2000, p. 359.
- ↑ UHJ 1972.
- ↑ World 1995.
- ↑ http: name=BWC//news.bahai.org/story/950
- ↑ Jumuiya ya Kimataifa ya Wabahá'í (2013-04-29). "Wabahá'í wachagua Nyumba ya Haki ya Ulimwengu". Huduma ya Habari ya Ulimwengu ya Wabahá'í. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-05-05. Iliwekwa mnamo 2013-05-01.
- ↑ Jumuiya ya Kimataifa ya Wabahá'í (2013-04-30). "Nyumba ya Haki ya Ulimwengu Yachaguliwa". Huduma ya Habari ya Ulimwengu ya Wabahá’í. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-07-06. Iliwekwa mnamo 2013-04-30.
- ↑ "Mkutano wa 13 wa Kimataifa: Wawakilishi kutoka nchi 176 walipiga kura kuchagua Nyumba ya Haki la Ulimwengu | BWNS". Huduma ya Habari ya Ulimwengu ya Bahá’í (kwa Kiingereza). 2023-04-29. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-05-21. Iliwekwa mnamo 2023-07-17.
- ↑ i24NEWS (2023-05-01). "Zaidi ya wawakilishi 1,300 wakusanyika kutoka nchi 170 kwa ajili ya mkutano wa Bahá'í nchini Israel". I24news (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-07-17. Iliwekwa mnamo 2023-07-17.
{{cite web}}
: CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ 15.0 15.1 15.2 15.3 Momen 1989.
- ↑ Baháʼu'lláh 1994, p. 125.
- ↑ 17.0 17.1 17.2 17.3 Smith 2000, pp. 350.
- ↑ "Ridván Messages". Baháʼí International Community. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Machi 2023. Iliwekwa mnamo 30 Machi 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Smith, Todd (2021-11-26), "The Writings of the Universal House of Justice", The World of the Bahá'í Faith (kwa Kiingereza) (tol. la 1), London: Routledge, uk. 151, doi:10.4324/9780429027772-14, ISBN 978-0-429-02777-2, iliwekwa mnamo 2023-07-17
- ↑ "13th International Convention: Universal House of Justice elected | BWNS". Bahá’í World News Service (kwa Kiingereza). 2023-05-01. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-06-04. Iliwekwa mnamo 2023-07-17.
- ↑ Smith 2000, p. 347.
- ↑ "Douglas Martin, 1927–2020". Baháʼí World Centre. Baháʼí World News Service. 2020-09-29. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-20. Iliwekwa mnamo 2020-10-18.
- ↑ "Obituary: Douglas Martin 1927 – 2020". The Globe and Mail. 2020-10-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-19. Iliwekwa mnamo 2020-10-18.
born February 24, 1927, and raised in Chatham, Ontario... passed away [Toronto, Ontario] ... September 28, 2020... Elizabeth, his wife, passed away in 1999. He leaves no children... In 1993, he was elected to ... Universal House of Justice, serving until his retirement in 2005. ... co-authored, with Dr. William Hatcher, "The Baháʼí Faith: The Emerging Global Religion"
- ↑ "Farzam Arbab, 1941–2020 | BWNS". Bahá’í World News Service (kwa Kiingereza). 2020-09-26. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-09. Iliwekwa mnamo 2020-09-27.
- ↑ "Two members of Universal House of Justice leaving after years of service". Baháʼí World News Service. 23 Aprili 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-13. Iliwekwa mnamo 2017-07-23.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Smith, Todd (2022). "Ch. 11: Nyumba ya Haki ya Ulimwengu". Katika Stockman, Robert H. (mhr.). Dunia ya Imani ya Kibahá’í. Oxfordshire, Uingereza: Routledge. ku. 134–144. ISBN 978-1-138-36772-2.
- Baháʼu'lláh (1994) [Imeandikwa 1873–92]. Tableti za Baháʼu'lláh Zilizo Funuliwa Baada ya Kitáb-i-Aqdas. Wilmette, Illinois, Marekani: Baháʼí Publishing Trust. ISBN 0-87743-174-4.
- Baháʼí International Community (2018-04-30). "Nyumba ya Haki ya Ulimwengu Imechaguliwa". Huduma ya Habari ya Ulimwengu ya Baháʼí. Iliwekwa mnamo 2018-05-25.
- The Baháʼí World 1993–94: rekodi ya kimataifa. Kituo cha Ulimwengu cha Baha'i. 1995. uk. 51. ISBN 0-85398-990-7.
- Momen, Moojan (1989). "BAYT-AL-ʿADL". Encyclopædia Iranica. Juz. la IV/1. ku. 12–14. Iliwekwa mnamo 2024-10-12.
- Smith, Peter (2000). "Nyumba ya Haki ya Ulimwengu". Ensiklopidia Fupi ya Imani ya Kibaháʼí. Oxford: Oneworld Publications. ku. 346–350. ISBN 1-85168-184-1.
- Nyumba ya Haki ya Ulimwengu (1972). "Katiba ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu". bahai.org. Iliwekwa mnamo 2018-09-05.
Usomaji wa ziada
[hariri | hariri chanzo]- Mkusanyiko (2021). Nyumba ya Haki ya Ulimwengu.
- Maktaba ya Bahai: Nyaraka zinazohusiana na Nyumba ya Haki ya Ulimwengu
- Schaefer, Udo (2000) [1999]. "Taasisisi zisizokosea?". Baháʼí Studies Review. 9. Iliwekwa mnamo 2014-09-29.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi
- Bahai.org: Ujumbe wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu
- Ujumbe wa Ridván – Rejeleo kamili la kihistoria (lugha nyingi)
- Ujumbe wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu (unajumuisha barua kwa Wabaháʼí wa Iran; kwa Kiingereza na Kiajemi)
- Ratiba ya Wanachama wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu