Nyoka-mbio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyoka-mbio
Nyoka-mbio majabali (Platyceps rhodorachis)
Nyoka-mbio majabali (Platyceps rhodorachis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Colubridae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Colubrinae (Nyoka wanaofanana na kipiri)
Oppel, 1811
Jenasi: Platyceps
Blyth, 1860
Ngazi za chini

Spishi 25:

Nyoka-mbio ni nyoka wa jenasi Platyceps katika familia Colubridae. Wamepewa jina hili kwa sababu wanaweza kupiga mbio sana.

Nyoka hawa ni wafupi kiasi, m 1.5 kwa kipeo lakini sm 40-90 kwa kawaida. Rangi yao ni kijivu au kahawia mara nyingi pamoja na vidoa au mabaka meusi.

Nyoka-mbio hukiakia mchana na hula mijusi hasa lakini vyura na ndege na wagugunaji wadogo pia.

Nyoka hawa hawana sumu lakini wakikamatwa wanang'ata vikali. Kwa hivyo jihadhari.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-mbio kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.