Nyansurumunti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Nyansurumunti ni kijiji kimoja kati ya vijiji vinne vinavyounda kata ya Kisaka katika wilaya ya Serengeti, mkoa wa Mara) ambavyo ni hicho pamoja na Borenga, Nyiboko na Buchanchari.

Kijiji hiki kimepakana na kijiji cha Buchanchari kwa upande wa mashariki. Kwa upande wa kaskazini kimepakana na bonde la mto Mara.

Vitongoji vya kijiji hiki ni Nyanchoka, Machita, Kobetimo, Kobiroga na Machegechege.

Wakazi wa kijiji hiki ni kabila la Wangoreme.

Kwa upande wa maendeleo kijiji hiki hakipo nyuma sana ukilinganisha na Borenga na Nyiboko ambavyo vimepiga hatua zaidi ya maendeleo.

Wakazi wengi wa kijiji ni wakulima na hulima mahindi (katika bonde la mto Mara), mtama, ulezi, viazi na mhogo kwa ajili ya chakula.

Kijiji hiki kina koo za Waghitare, Wabhusawe, Wanguku n.k.

Vyama vya siasa vinavyotesa katika kijiji hiki ni CCM, Chadema & CUF.

Mwaka 2014 chama tawala katika kijiji hiki kilikuwa CCM. Kikabadilika kuwa Chadema mwaka wa 2015.

Baadhi ya wanasiasa maarufu katika kijiji hicho ni Thobias Makindi na Mwikwabe Chacha.

Baadhi ya wenyeviti waliowahi kuongoza kijiji hiki ni Mwikwabe Chacha Wandera, Anicet Makori, Saghi Kitang'ita Saghi n.k.

Pia kijiji kima timu ya mpira wa miguu iitwayo Nyuki Sports Club.

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyansurumunti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.