Nyanda za juu za Yunnan–Guizhou
Mandhari
Nyanda za juu za Yunnan-Guizhou ni eneo katika kusini magharibi ya China. Kanda hii inaenea hasa katika majimbo ya Yunnan na Guizhou.
Upande wa kusini tabia yake ni zaidi kama tambarare ya juu lakini kaskazini kuna milima. Kwa jumla zinapakana na nyanda za juu za Tibet upande wa magharibi-kaskazini.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Kwa jumla nyanda za juu huwa kwenye kimo cha mita 1,000 hadi 2,000 juu ya usawa wa bahari. Kwa muda mrefu eneo hilo limezingatiwa kuwa nyuma kiutamaduni na kiuchumi nchini China. [1] Wakazi wengi wanaishi kwa mtindo wa jadi katika vijiji.
Nyanda hizo zinatenganisha mabeseni ya mito mikubwa kama vile Yangzte, Xi Jiang na Yuan Jiang.[2] [3]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ China's Southwest. Lonely Planet. 2007. ISBN 9781741041859.
- ↑ Atlas of China. Beijing, China: SinoMaps Press. 2006. ISBN 9787503141782.
- ↑ Suettinger, Robert Lee. "Yunnan". Encyclopædia Britannica. Encyclopædia Britannica, Inc. Iliwekwa mnamo 31 Agosti 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Expansion of the Chinese Paddy Rice to the Yunnan-Guizhou Plateau Ilihifadhiwa 27 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nyanda za juu za Yunnan–Guizhou kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |