Novatus Dismas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Novatus Dismas Miroshi
Maelezo binafsi
Tarehe ya kuzaliwa 2 Septemba 2002
Mahala pa kuzaliwa    Tanzania
Nafasi anayochezea Kiungo wa kati
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Shaktar Donesk
Timu ya taifa
Timu ya Taifa ya Tanzania

* Magoli alioshinda

Novatus Dismas Miroshi (alizaliwa 2 Septemba 2002) ni mchezaji wa soka wa nchini Tanzania ambaye anachezea katika klabu ya SV. Zulte Waregem, Ubelgiji na Timu ya Taifa ya Tanzania.

Klabu[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2022, Dismas alisaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya SV. Zulte Waregem huko Ubelgiji.[1]

Ushiriki Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Dismas alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa katika timu ya taifa ya soka ya Tanzania chini ya miaka 20 mnamo 16 Februari 2021 katika mchezo wa mechi ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika U-20 ambapo timu ya taifa ya soka ya Ghana chini ya miaka 20 ilishindwa kwa mabao 4-0. Mnamo 19 Februari, alifunga bao lake la kwanza kwa katika timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya timu ya taifa ya soka ya chini ya miaka 20 ya Gambia katika mechi iliyotoka sare kwa bao 1 - 1.

Mnamo 2 Septemba 2021, Dismas alicheza katika mechi ya timu ya taifa ya soka ya Tanzania katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya soka ya DR Congo katika mechi ya kufuzu ya Kombe la Dunia 2022.[2] Mnamo 7 Septemba, alifunga bao lake la kwanza katika ushindi wa mabao 3 - 2 dhidi ya timu ya taifa ya soka ya Madagaska.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Novatus Miroshi is trots om boer te zijn (nl). Zulte Waregem (22 August 2022).
  2. FIFA (en).
  3. FIFA (en).
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Novatus Dismas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.