Nenda kwa yaliyomo

Norovirus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Norovirus
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuDawa ya dharura, ugonjwa wa watoto
DaliliKuhara, kutapika, maumivu ya tumbo, maumivu ya kichwa[1]
Muda wa kawaida wa kuanza kwakeSaa 12 hadi 48 baada ya kuambukizwa[1]
MudaSiku 1 to 3[1]
VisababishiNorovirus[2]
Njia ya kuitambua hali hiiKulingana na dalili[2]
KingaKunawa mikono, kuuwa virusi kwenye maeneo yaliyoambukizwa[3]
MatibabuHuduma ya kusaidia (kunywa maji ya kutosha au viowevu vya kupitia kwa mishipa)[4]
Idadi ya utokeaji wakeMatukio milioni 685 kwa mwaka[5]
Vifo200,000 kwa mwaka[5][6]

Norovirus (wakati mwingine hujulikana kama mdudu wa kutapika wakati wa baridi) ni sababu ya kawaida ya kuvimba kwa tumbo na matumbo (gastroenteritis).[7][5]

Maambukizi yake yanaonyeshwa na kuhara ambako hakuna damu, kutapika na maumivu ya tumbo.[1][2] Homa au maumivu ya kichwa yanaweza pia kutokea.[1] Dalili zake za kawaida hutokea masaa 12 hadi 48 baada ya kuambukizwa, na ahueni kwa kawaida hutokea ndani ya siku 1 hadi 3.[1] Matatizo hayatokei kwa kawaida, lakini yanaweza kujumuisha upungufu wa maji mwilini, hasa kwa vijana, wazee, na wale walio na matatizo mengine ya afya.[1]

Kwa kawaida virusi hivi huenezwa kwa njia ya vijidudu (virusi, bakteria, au vimelea) kutoka kwa kinyesi cha mtu aliyeambukizwa kuingia mwilini kupitia mdomo.[2] Hili linaweza kuwa kupitia chakula au maji yaliyochafuliwa au kuwasiliana na mtu hadi mtu.[2] Ugonjwa huu unaweza pia kuenea kupitia nyuso zilizochafuliwa au kupitia hewa kutoka kwa matapishi ya mtu aliyeambukizwa.[2] Sababu za hatari ni pamoja na utayarishaji wa chakula usio safi na kushiriki maeneo ya karibu.[2] Utambuzi wake kwa ujumla hutegemea dalili.[2] Upimaji wa uthibitisho wake kwa kawaida haupatikani, lakini unaweza kufanywa wakati wa milipuko na mashirika ya afya ya umma.[2]

Kinga dhidi yake inahusisha kunawa mikono kwa usahihi na kuondoa maambukizo kwenye nyuso zilizochafuliwa.[3] Vitakaso vya mikono vinavyotokana na pombe vinaweza kutumika kwa kuongeza, lakini havina ufanisi kuliko kunawa mikono.[3] Hakuna chanjo au matibabu maalumu ya norovirus.[3][4] Usimamizi wake bora unahusisha utunzaji wa usaidizi kama vile kunywa viowevu vya kutosha au viowevu vya kupitia ndani ya mishipa.[4] Viowevu vya urejeshaji maji mwilini ndivyo vinywaji vinavyopendekezwa kunywewa, ingawa vinywaji vingine visivyo na kafeini au pombe vinaweza kusaidia.[4]

Norovirus husababisha takriban matukio milioni 685 vya magonjwa na vifo 200,000 ulimwenguni kote kwa mwaka.[5][6] Ni kawaida katika ulimwengu ulioendelea na unaoendelea.[2][8] Wale walio chini ya umri wa miaka mitano huathirika zaidi, na katika kundi hili husababisha vifo 50,000 hivi katika ulimwengu unaoendelea.[5] Maambukizi ya Norovirus hutokea mara nyingi zaidi wakati wa miezi ya baridi.[5] Mara nyingi hutokea katika milipuko, hasa kati ya wale wanaoishi katika maeneo ya karibu.[2] Nchini Marekani, ugonjwa huu ndio sababu ya karibu nusu ya magonjwa yote yanayotokana na chakula.[2] Virusi hivi vimepewa jina la jiji la Norwalk, Ohio, ambapo mlipuko wake ulitokea mwaka wa 1968.[9]

  1. 1 2 3 4 5 6 7 "Norovirus Symptoms". CDC (kwa American English). 24 Juni 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Desemba 2018. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 Brunette, Gary W. (2017). CDC Yellow Book 2018: Health Information for International Travel. Oxford University Press. uk. 269. ISBN 9780190628611. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-29. Iliwekwa mnamo 2017-12-29.
  3. 1 2 3 4 "Preventing Norovirus Infection". CDC (kwa American English). 5 Mei 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 1 2 3 4 "Norovirus - Treatment". CDC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 1 2 3 4 5 6 "Norovirus Worldwide". CDC (kwa American English). 15 Desemba 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Desemba 2018. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 1 2 "Global Burden of Norovirus and Prospects for Vaccine Development" (PDF). CDC. Agosti 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 29 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Norovirus (vomiting bug)". nhs.uk. 2017-10-19. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-12. Iliwekwa mnamo 8 Juni 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Nguyen GT, Phan K, Teng I, Pu J, Watanabe T (Oktoba 2017). "A systematic review and meta-analysis of the prevalence of norovirus in cases of gastroenteritis in developing countries". Medicine. 96 (40): e8139. doi:10.1097/MD.0000000000008139. PMC 5738000. PMID 28984764.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Vesikari, Timo (2021). "25. Norovirus vaccines in pipeline development". Katika Vesikari, Timo; Damme, Pierre Van (whr.). Pediatric Vaccines and Vaccinations: A European Textbook (kwa Kiingereza) (tol. la Second). Switzerland: Springer. ku. 289–292. ISBN 978-3-030-77172-0. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-10-20. Iliwekwa mnamo 2023-10-05.