Nomvelo Makhanya
| Nomvelo Makhanya | |
|---|---|
Makhanya mnamo mwaka 2026 |
Nomvelo Makhanya[1] (aliyezaliwa tarehe 24 Aprili 1996) ni mwigizaji na mwimbaji kutoka Afrika Kusini ambaye ameshinda tuzo.Anajulikana zaidi kwa kuigiza katika vipindi vya runinga kama Isibaya, kwenye filamu ya Soul City na Scandal!. Pia hivi karibuni alijiunga na filamu ya Netflix iitwayo I Am All Girls.
Maisha Binafsi
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa 24 Aprili 1996 huko Nkandla, katika mkoa wa KwaZulu-Natal, nchini Afrika Kusini. Baada ya miaka michache, alihamia Johannesburg pamoja na wazazi wake.Mwaka 2016, aligundulika kuwa na msongo wa mawazo na wasiwasi. Hata hivyo, baada ya kupata ushauri nasaha mara kadhaa, aliweza kuondokana na hali hiyo.Mwezi Januari 2019, dereva mmoja aliyedaiwa kuwa alikuwa amelewa aligonga gari la Nomvelo lililokuwa limeegeshwa.Mwezi Februari 2019, Nomvelo alitoa ujumbe wa kueleza hisia zake kupitia mitandao ya kijamii. Alisema kuwa alikuwa akinyanyaswa na kudhalilishwa mtandaoni kwa sababu ya muonekano wa kichwa chake[2].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Peris Walubengo (2022-12-14). "Nomvelo Makhanya's biography: age, career, boyfriend, parents, Scandal - Briefly.co.za". briefly.co.za (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-09-26.
- ↑ Nkosazana Ngwadla. "Scandal! actress Nomvelo Makhanya on being cyberbullied: "I know I'm beautiful"". News24 (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-09-26.
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nomvelo Makhanya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |