Noemi (mwimbaji)

Veronica Scopelliti (alizaliwa Januari 25, 1982),[1] anayejulikana kitaaluma kama Noemi, ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo wa Italia.[2] Tangu alipopata umaarufu mkubwa baada ya kushiriki katika msimu wa pili wa shindano la kusaka vipaji la Italia la X Factor mnamo mwaka 2009, ametoa albamu saba za studio, zilizopitishwa na nyimbo zilizopata mafanikio makubwa ya kibiashara kama vile 'Briciole', 'Vuoto a perdere', 'Per tutta la vita', pamoja na nyimbo zake zilizoshindanishwa kwenye Tamasha la Muziki la Sanremo za 'Sono solo parole', 'Glicine', 'Ti amo non lo so dire', na 'Se t'innamori muori.[3]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Noemi alizaliwa mnamo Januari 25, 1982, Roma, akiwa binti mkubwa wa Armando na Stefania. Baba yake alikuwa mjasiriamali, kisha akaja kuwa diwani wa jiji (city councilor) huko Vasto, wakati mama yake alikuwa mchoraji.Wote wawili walijaribu kujenga taaluma katika tasnia ya muziki, ambapo Armando alishiriki katika Tamasha la Muziki la Castrocaro, na Stefania alikuwa akitumbuiza kama mwimbaji chipukizi (amateur singer).[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.piazzarossetti.it/it-it/notizie/5156b8ecd199709005009dc4/i-vastesi-ricordano-armando-scopelliti-il-papa-della-cantante-noemi
- ↑ https://dilei.it/star-e-vip/noemi/
- ↑ https://www.corriere.it/sette/18_aprile_26/ho-cantato-bar-pizzerie-questo-sono-preparata-e8b53e22-47c5-11e8-80f7-0314029e9b8f.shtml
- ↑ https://italiancharts.com/showitem.asp?interpret=Noemi+%5BIT%5D&titel=Briciole&cat=s
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Noemi (mwimbaji) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |