Nkulunkulu Mnikati wetibusiso temaSwati
Nkulunkulu Mnikati wetibusiso temaSwati ni wimbo wa taifa wa Eswatini. Wimbo huu unachanganya mitindo ya muziki wa jadi wa Waswati na muziki wa Magharibi. Ulipitishwa rasmi mwaka 1968, baada ya nchi hiyo kupata uhuru. Mashairi yake yaliandikwa na Andrease Enoke Fanyana Kukies Simelane, huku mtunzi wa ala (melodi) akiwa David Kenneth Rycroft.[1][2][3][4][5]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Wakati Eswatini (iliyokuwa ikijulikana kama Swaziland) ilipokuwa ikijiandaa kupata uhuru kutoka Uingereza tarehe 6 Septemba 1968, serikali iliamua kupitisha bendera mpya na kutafuta wimbo wa taifa. Iliundwa kamati maalumu na kutangazwa mashindano ya kutunga mashairi kwa lugha ya siSwati pamoja na mashindano ya kutunga melodi ya wimbo huo.
Baada ya kupokea mapendekezo mengi, majaji walichagua melodi nne bora. Nyimbo hizo ziliimbwa kwanza na kwaya nchini Afrika Kusini, kisha zikaimbwa tena na kwaya ya Waterford School mjini Mbabane ili Baraza la Mawaziri lifanye uamuzi wa mwisho.
Hatimaye, melodi iliyotungwa na David Kenneth Rycroft ilichaguliwa kuwa wimbo wa taifa. Mashairi yake yaliandikwa na Andrease Fanyana Kukies Simelane. Kabla ya siku ya uhuru, wimbo huo ulianza kurushwa kila siku kupitia Radio Swaziland ili kuwapa wananchi nafasi ya kujifunza.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Swaziland". nationalanthems.info. Iliwekwa mnamo 2009-10-04.
- ↑ Dlamini, Betty Sibongile (2010). Asikhulume SiSwati (kwa Kiingereza). University of Wisconsin-Madison. uk. 226. ISBN 978-1-59703-018-2.
- ↑ African Language Studies (kwa Kiingereza). School of Oriental and African Studies, University of London. 1970. ku. 288–301.
- ↑ "Who we are". The Government Of the Kingdom Of Eswatini. Iliwekwa mnamo 2022-01-18.
- ↑ Ginindza, Zodwa R. (1986). Umntfwana!: A Pictorial Biography of the New King of Swaziland (kwa Kiingereza). Macmillan Swaziland National Publishing Company. ISBN 978-0-333-40303-7.
| Makala hii kuhusu muziki wa Afrika bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nkulunkulu Mnikati wetibusiso temaSwati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |