Nkem Owoh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nkem Owoh

Amezaliwa Nkem Owoh
Enugu Nigeria
Kazi yake Muigizaji

Nkem Owoh ni muigizaji na mchekeshaji wa Nigeria. Mwaka 2008 alishinda tuzo ya African Movie Academy Award kama Muigizaji Bora katika sehemu ya uongozi. [1]

Maisha Yake ya Utotoni[hariri | hariri chanzo]

Owoh alizaliwa Enugu Nigeria Baada ya masomo yake ya msingi na ya upili, alienda Chuo Kikuu cha Ilorin alikosomea uhandisi. Kama bado anasoma masomo ya chuo kikuu, Owoh alianza uigizaji katika televisheni na filamu.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Owoh alikuwa kati ya waigizaji wakuu katika filamu ya 2003 ya Osuofia i London . Anajulikana pia kwa kuuimba wimbo wa I Go Chop Your Dollar, unaohusu ufisadi wa ada ya mapema. Wimbo huu ulitumika katika filamu ya The Master ambapo Owoh hucheza kama mtapeli.[2] Tume ya Uhalifu wa Fedha na Uchumi na Tume ya Utangazaji ya Nigeria ilipiga marufuku wimbo huo[3]. Mwaka 2007 alikamatwa na polisi mjini Amsterdam, Uholanzi(kitongoji Bijlmermeer katika eneo la Amsterdam Zuidoost) kama matokeo ya uchunguzi wa miezi 7 ulioitwa "Operation Apollo".[2] Owoh alikuwa akitumbuiza wakati polisi walivamia pahali pale na kuwatia mbaroni watu 111 kwa tuhuma za udanganyifu makosa ya uhamiaji. Owoh baadaye aliachiliwa huru.[3][4][5] Mwezi Novemba 2009, Owoh alitekwa nyara eneo la mashariki mwa Nigera. Wateka nyara walitaka naira milioni 15 kama makombozi. Aliachiliwa huru baada ya familia yake kutoa naira milioni 1.4 kama makombozi.

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Filamu Jukumu Vidokezo
1987 Things fall apart na Pete Edochie
1995 Ukwa na Patience Ozokwor
1999 Big Man...Big Trouble
Conspiracy na Onyeka Onwenu
2001 Onye-Eze Onye-Eze
2002 Fake Doctor Dr. Zebedi
Ifeonye metalu
Long John
Police Officer
Spanner na Chinedu Ikedieze
2003 Anunuebe
King of the Forest
Lion Finger
Mr. Trouble na Patience Ozokwor
Osuofia in London
Police Recruit
2004 America Visa
My Driver
My Own Share
Osuofia in London 2
Spanner Goes to Jail na Chinedu Ikedieze
2005 Akanchawa
Bus Driver na Dakore Egbuson
The Prince
2006 A Fool at 40 Hygenius
Captain
Foreign Base
Indemnity Egbentu
Made in Cambridge
My Kingdom Come
The Barrister Athanasius
The Dreamer
2007 Battle of Indemnity Egbentu
Covenant Keeping God Samuel
De prof
Johnbull & Rosekate Johnbull
Persecution
Stronger Than Pain Ulonna na Kate Henshaw-Nuttal
Uigizaji wake katika filamu hii ulifanya apewe tuzo la Best Actor in a Leading Role
katika African Movie Academy Awards mwaka 2008
2008 His Holiness
His Last Action
Wonderful Man

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. AMAA 2008: List of Winners. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-11-26. Iliwekwa mnamo 2009-11-11.
  2. 2.0 2.1 Jan Libbenga (2007-07-02). 'I Go Chop Your Dollar' star arrested. The Register.
  3. 3.0 3.1 Police Arrest Nkem Owoh in Holland. NigeriaMovies.net (2007-07-04). Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2009-12-23.
  4. 'I Go Chop Your Dollar' star arrested. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-07-16. Iliwekwa mnamo 27 Novemba 2009.
  5. | Jan Libbenga (2021-03-30). I Go Chop Your Dollar star arrested

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]