Nenda kwa yaliyomo

Njoki Wamai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Njoki Wamai ni msomi, mwanaharakati wa kifeministi, na mfuasi wa Pan-Africanism kutoka Kenya ambaye kazi yake imejikita katika masuala ya watu waliotengwa, haki za binadamu, haki ya mpito baada ya migogoro, haki za wanawake na siasa za Afrika, akitumia mitazamo ya ki-critical, kifeministi na kidekolonial.[1][2]

Yeye ni mhadhiri msaidizi katika Idara ya Mahusiano ya Kimataifa katika United States International University Africa (USIU-A) jijini Nairobi.[3] Mwaka 2016 alitunukiwa tuzo ya Bill Gates Sr. Prize kwa uongozi na mchango wake ndani ya jamii ya Gates Cambridge.[4][5]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Njoki Wamai alipata Shahada ya Sayansi katika chakula na teknolojia pamoja na Diploma ya Uzamili katika Jinsia na Maendeleo kutoka chuo kikuu cha Nairobi.[1][6]

Baadaye alikamilisha Shahada ya Uzamili katika Migogoro, Ulinzi na Maendeleo katika King's College London kupitia African Leadership Centre, na kuhitimu kwa daraja la juu (distinction).

Alipata Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Siasa na uhusiano wa kimataifa kutoka chuo kikuu cha Cambridge mwaka 2017 akiwa Gates Cambridge Scholar.[7]

Baada ya PhD, alifanya utafiti wa baada ya udaktari katika Centre for Governance and Human Rights (CGHR) ya Cambridge.[8]

Kazi na utafiti

[hariri | hariri chanzo]

Njoki Wamai ni mhadhiri msaidizi wa Mahusiano ya Kimataifa katika USIU-A Nairobi, ambapo hufundisha na kufanya utafiti kuhusu haki za binadamu, siasa za Afrika na maendeleo ya kimataifa.[9]

Utafiti wake unachunguza uhusiano kati ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) na mifumo ya haki ya ndani barani Afrika.[5]

Amefanya kazi na mashirika ya kiraia ikiwemo Kenya Human Rights Commission na Centre for Humanitarian Dialogue.[7] Pia amechangia katika sera za kitaifa za Kenya kuhusu Wanawake, Amani na Ulinzi.[5]Njoki Wamai amechangia mijadala ya umma kupitia The Conversation, The Elephant, HuffPost na Pambazuka News pamoja na vyombo vingine vya habari.

Ushirikiano na tuzo

[hariri | hariri chanzo]

Yeye ni mjumbe wa bodi ya Life & Peace Institute.[3] Pia ni alumna wa African Leadership Centre ya King's College London. Akiwa Cambridge alianzisha Black Cantabs Research Society, mradi wa kurekodi historia ya watu Weusi katika chuo hicho na kupinga kufutwa kwa mchango wao.[10] Mwaka 2024 alitajwa miongoni mwa Wanawake 100 Bora wa Kitaaluma Afrika.[11]

  1. 1 2 "The ASSN Quarterly – October 2012" (PDF). African Security Sector Network. Oktoba 2012. Iliwekwa mnamo 22 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. ↑ "Wamai, Njoki (PhD)". United States International University Africa. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)[dead link]
  3. 1 2 "Our People". Life & Peace Institute. Iliwekwa mnamo 22 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. ↑ "Kenyan Njoki Wamai wins 4th Bill Gates Sr Prize". HerBusiness Kenya. 2016. Iliwekwa mnamo 22 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)[dead link]
  5. 1 2 3 "An Interview with Njoki Wamai". SSRC Kujenga Amani. Social Science Research Council. 18 Februari 2020. Iliwekwa mnamo 22 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. ↑ "Njoki Wamai – Fellow 2022/2023". Wissenschaftskolleg zu Berlin. Iliwekwa mnamo 22 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 1 2 "Njoki Wamai". Gates Cambridge. Iliwekwa mnamo 22 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. ↑ "Wamai, Njoki, PhD". USIU-Africa. Iliwekwa mnamo 22 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)[dead link]
  9. ↑ "Njoki Wamai Profile". Muck Rack. Iliwekwa mnamo 22 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. ↑ "Celebrating Black Cantabs". University of Cambridge. Iliwekwa mnamo 22 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. ↑ "Top 100 Career Women in Africa 2024". TVC News. 2024. Iliwekwa mnamo 23 Oktoba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)