Nenda kwa yaliyomo

Njideka Harry

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Njideka Françoise Harry ni mshirika (Fellow) wa World Economic Forum kupitia Schwab Foundation for Social Entrepreneurship.

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Harry alizaliwa mjini Ibadan akiwa na baba kutoka Nigeria na mama kutoka Marekani.[1] vita vya Biafra vilipoanza, baba yake alishinda ufadhili wa masomo kwenda kusoma Marekani, ambako ndipo alikutana na kumuoa mama yake.[2]

Alipata shahada ya kwanza ya Utawala wa Biashara katika Fedha na Uchumi kutoka University of Massachusetts Amherst.

Baada ya kuhitimu masomo, alianza kufanya kazi General Electric, akiishi na kufanya kazi Ulaya na Marekani. Baadaye, Harry aliacha kazi GE na kuanza kazi Microsoft, ambako alianzisha shirika la YTF mwaka 2000, Shirika hilo lisilo la kiserikali hutumia teknolojia kuboresha maisha ya vijana na wanawake katika nchi zinazoendelea.

Harry ana wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya elimu barani Afrika, akisema kuwa mfumo wa elimu haujavunjika tu bali pia umepitwa na wakati. Anaiona teknolojia kama nyenzo muhimu ya kuwezesha mabadiliko chanya.[3][4]

  1. "NJIDEKA HARRY'S QUEST TO MAKE THE STATE AND OUTCOME OF RURAL FARMING APPEALING TO RURAL WOMEN | Aim Higher Africa". aimhigherafrica.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2018-08-06.
  2. Harry, Njideka (2015). "Pioneering the Youth and Technology Movement in Africa and Beyond (Case Narrative)". Innovations: Technology, Governance, Globalization (kwa Kiingereza). 10 (1–2): 61–73. doi:10.1162/inov_a_00230. ISSN 1558-2477.
  3. Journo, Pro (2013-04-15). "Youth for Technology Foundation: Reinvigorating Rural Communities through Reverse Migration & Youth Empowerment". Huffington Post (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-08-06.
  4. Wall, Matthew (2014-07-01). "Africa mobile boom powers innovation". BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2018-08-06.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Njideka Harry kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.