Nina Sky

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nina Sky
Nina Sky
Nina Sky
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii Nina Sky
Nchi Marekani
Alizaliwa 13 Machi 1986
Aina ya muziki R&B, Hip-Hop, Reggaeton
Kazi yake Wanamuziki
Miaka ya kazi 2004 – mpaka leo
Kampuni Universal (2004–2007)

Polo Grounds / J (2007–mpaka leo)

Nicole na Natalie Albino (wamezaliwa tar. 13 Machi 1986 mjini Queens, New York) ni wanamuziki wa raggae riddim na R&B-ndugu mapacha wajulikanao kwa jina la "Nina Sky".

Maisha ya awali na kazi ya muziki[hariri | hariri chanzo]

Wazazi wao walihamia mjini New York wakitokea nchini Puerto Rico na si-muda toka wa hamie huko wakatarikiana, watoto wakiwa wangali wadogo. Walikulia mjini Queens na kisiwani Roosevelt ambayo pia ni sehemu ya New York.

Kutokana na babao wa kufikia alikuwa akifanya kazi ya U-dj, watoto hao wakawa wamevutiwa na aina tofauti ya muziki. Wakiwa wana umri wa miaka 7, wakajaribu kuandika nyimbo zao wenyewe kwa mara ya kwanza, na wimbo ulikwenda kwa jina la "Ndugu", na walipofika umri wa maiaka kumi, wakawa washajua kama wao wanataka kuwa wanamuziki.

Wazazi wa watoto hao walikuwa wakitoa msaada mkubwa na hata kuwapa matumaini ya ndoto walizonazo watoto wao. Babao wa kufikia alithubutu hata kuwapa gita na ngoma na kuwapa baadhi ya mafunzo yahusianayo na vitu hivyo. Walikuwa wakifanya nyimbo kisha wanampelekea msikilizaji ajaribu kutoa tathimini ya nyimbo zao na kipindi hicho hicho wakawa wanapata vijitamasha vya mtaani.

Toka hapo wakawa wanafanya mpango wa kubuni jina watakalokuwa wanalitumia wakiwa kama wasanii. Ikawalazimu watumie silabi mbili za majina yao (1 "Ni" na 2 "Na"), wakatoka na jina liitwalo Nina. Na kisha baadae wakaongeza Sky, ambalo wao walikuwa wakiwakilisha "sky's the limit".

Kipindi chote hicho walikuwa bado wakindelea na masomo, na wakipata muda wa akiba walikuwa wakifanya kazi ya U-dj. Kunako mwaka wa 2000, walikutana na The Jettsonz (Elijah Wells na Lionel Bermingham), ni moja wa waandaaji muziki na ndiyo walio wasaidia kuweza kufanya kazi ya muziki rasmi.

Mwanzo wa kupata mafanikio[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka wa 2004, The Jettsonz waliwatambulisha wadada hao kwa Cipha Sounds, na akawachukua mpaka katika studio inayomilikiwa na kikundi cha muziki aina ya hip hop "The Neptunes" (yaani Pharrell Williams na Chad Hugo). Cipha Sounds alivutiwa sana na sauti za madada hao na akashauri kwamba wadada hao waimbe ule mtindo unaoitwa raggae riddim au kwa jina lingine "Coolie Dance".

Ndugu hao waliendelea kuandika mashairi yao na wakafanikiwa kutoa kibao kimoja kiitwacho "Move Ya Body" (wakishirikiana na The Jettsonz, ambaye pia walisshiriki kutayarisha wimbo huo). Nyimbo ilichanganya mandhari tofauti kidoogo, walichanganya kidogo riddim za Kikaribi na R&B.

Kwa bahati nzuri nyimbo hiyo ya kwanza ilifanya vizuri. Nyimbo ilitamba na hadi kufikia mikononi mwa mmiliki wa Next Plateau Entertainment bwana Eddie O'Loughlin (pia ni moja ya sehemu ya Universal Records). O'Loughlin aliingia nao mkataba wa kurekodi albamu ya kwanza na hapo ndipo mafanikio yalipo anza.

Albamu walizotoa[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu ya: Albamu za Nina Sky

Albumu[hariri | hariri chanzo]

  1. 2004: Nina Sky
  2. TBA: The Musical

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.dominicantimes.com/news.php?nid=425
  2. http://www.sing365.com/music/lyric.nsf/Nina-Sky-Biography/76AE7A1B3112B98C48256ECB0005E791
  3. http://music.yahoo.com/ar-308196---Nina-Sky

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: