Nikola Mektić
Mandhari
Nikola Mektić (Alizaliwa 24 Desemba, 1988) ni mchezaji wa tenisi nchini Kroatia. Alikuwa mchezaji namba 1 duniani katika mechi za wachezaji wawili (doubles). Alishinda mataji mawili ya Grand Slam: Wimbledon mwaka 2021 katika mechi za wachezaji wawili kwa kushirikiana na Mate Pavić. Alicheza mechi za wachezaji mchanganyiko (mixed doubles) akishirikiana na Barbora Krejčíková katika Australian Open ya mwaka 2020.[1]
Mektić alizaliwa Zagreb, Kroatia (zamani Yugoslavia) mwaka 1988. Alianza kucheza tenisi akiwa na umri wa miaka 6. Mwaka 2021, alishinda medali ya dhahabu katika Olimpiki akiwa na Pavić, na kuwa mchezaji wa kwanza wa Kroatia kushinda dhahabu katika tenisi ya Olimpiki.[2]