Nice Githinji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nice Githinji (amezaliwa 25 Agosti 1985) [1] ni mwigizaji wa filamu, mhudumu wa karaoke na muandaaji wa filamu na wa vipindi vya televisheni nchini Kenya.

Anafahamika sana kwa kufanya majukumu mbalimbali kwenye televisheni. Alipata umaarufu zaidi aliposhiriki katika tuzo za Kalasha mnamo mwaka 2009, katika kinyang’anyiro cha mwigizaji bora wa kike wa filamu inayoitwa Girls Together mnamo mwaka 2011. [2] Baadae alishinda tuzo ya kuwa mwigizaji bora wa maigizo kuhusu majukumu yake ya kila siku kwenye televisheni inayojulikana kwa jina la Changing Times. .[3][4] Licha tu ya kuwa mwigizaji, pia ni mwanzilishi wa Nicebird Production company inayohusika na kuandaa filamu. [5]

Amefanya kazi Et Cetera Productions (2007-2008: ambapo alikua mhusika mkuu wa filamu mbili ,zilizojulikana kwa majina ya , Benta and All Girls Together, Sisimka Productions and Phoenix Players (2009-2010) na Planet’s Theatre.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Nice alizaliwa mnamo mwaka 1985jijini Mombasa. Alisoma masomo yake ya sekondari katika shule ya Senior Chief Koinange High School kuanzia mwaka 1999 hadi 2002.[6] Her mother died when she had finished high school.[7]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya awali na uanzilishi wa showbiz[hariri | hariri chanzo]

Nice Githinji alianza kazi yake ya uigizaji katika majukwaa, alianza kwa kuigiza katika kazi ya Phoenix Players iliyoratibniwa na bwana Richard Stockwell kwa jina la Bad Blood, uhusika huo ulisukuma kwa kasi kuanza kwake kuigiza. Amejitokeza katika filamu na maonyesho ya televisheni mbalimbali.

2007  – 2009[hariri | hariri chanzo]

Kati ya miaka 2007 na 2010, aliigiza katika filamu mbalimbali kama; Benta, All Girls Together, Formula X na Pieces of Peace.[8] pia alikua mhusika mkuu katika maonyesho ya televisheni kama kama; Guy Centre na Changing Times ambamo alijulikana kwa majina ya Candy na Rosa.

Sanaa[hariri | hariri chanzo]

Filamu na Televisheni[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Kazi Uhusika Maelezo
2007 Benta Sheana Akiwa na Janet Kirina
2008 All Girls Together Sasha Ni mtayarishaji
Formular X Cindy
Unseen, Unsung, Unforgotten Rita
Pieces of Peace Wairimu Filamu inayoelezea machafuko ya kisiasa Kenya yam waka 2007-08
2009 Guy Centre Candy
2010  – 2012 Changing Times Rosa Mhusika Mkuu
2010 Kidnappet Lilly
2011 Saints Nesi Millicent
2012 Better Days Nelly
2012 Consequences
2013 mpaka sasa African Urban Entertainment Muendesha kipindi
2013 House of Lungula Charity Filamu
2014 East
Home
Six
Flowers and Bricks
2015 How to Find a Husband
2016 hadi sasa Makutano Junction Toni Kachukua uhusika wa Wanja Mworia kuanzia sehemu ya 15
2016 – 2017 Tumaini Senta Taabu Uhusika mkuu
2017- The Squad Akiwa peke yake Mwanachama[9]
2018 Rafiki Nduta


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nice Githinji's biography". actors.co.ke. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-26. Iliwekwa mnamo October 29, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Previous winners". Kalasha Awards. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 July 2013. Iliwekwa mnamo 7 January 2016.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  3. "2011 Kalasha awards winners". Actors.co.ke. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-09. Iliwekwa mnamo 7 January 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. Capital Lifestyle (11 September 2011). "Vote for your 3rd edition Kalasha Awards winners". Capital FM. Iliwekwa mnamo 7 January 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. "Nice Githinji- LinkedIn". LinkedIn. Iliwekwa mnamo 7 January 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  6. "Nice Githinji-Linked In". LinkedIn. Iliwekwa mnamo 7 January 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  7. David Koech (29 September 2014). "10 Things You Did Not Know About Nice Githinji". Nairobi Wire. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-21. Iliwekwa mnamo 7 January 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  8. "Nice Githinji: Wasanii". Wasanii. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 7 January 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  9. "The New All Female Cast TV Talk Show Dubbed The Squad", Diaspora Messenger News Media, 2017-01-09. (en-US)