Nenda kwa yaliyomo

Nia Long

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nia Long

Mshindi wa tuzo tatu za NAACP Image Awards
Amezaliwa Nia Talita Long
30 Oktoba 1970 (1970-10-30) (umri 55)
New York City, U.S.
Nchi Marekani
Majina mengine Nia Talita Long
Kazi yake Mwigizaji
Kipindi 1986–sasa
Watoto 2
Mahusiano Ime Udoka (2010–2022)

Nia Talita Long (amezaliwa Oktoba 30, 1970) ni mwigizaji wa Marekani. Anajulikana zaidi kwa kazi zake katika filamu zinazohusu maisha ya watu weusi nchini Marekani ,[1] Long alipata umaarufu baada ya kuigiza katika filamu ya Boyz n the Hood (1991), na alishiriki kwa uhusika wake kama Beullah "Lisa" Wilkes kwenye kipindi cha vichekesho cha NBC, The Fresh Prince of Bel-Air (1991–1995).

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Long alizaliwa mnamo Oktoba 30, 1970, huko Brooklyn ambaye baba yake ni Talita Long, mwalimu na mchapishaji,[2] na mama yake Doughtry Long, mwalimu wa shule ya sekondari na mshairi. Mama yake ni mwenye asili ya Trinidad. Long ana dada mkubwa wa kambo, ambaye ni mwigizaji na mchekeshaji maarufu kwa jina la Sommore. Alihitimu katika Shule ya sekondari ya Westchester huko Los Angeles mnamo 1989.[3]

Mwalimu wa uigizaji aliyemfundisha Long alikuwa Betty Bridges. Uhusika wake wa kwanza kwenye televisheni ulikuwa kama Kathryn "Kat" Speakes kwenye igizo la (soap opera) la Guiding Light kuanzia mwaka 1991 hadi 1994. Kuanzia mwaka 1994 hadi 1995, alicheza kama mpenzi na mchumba wa Will Smith, Beulah "Lisa" Wilkes, kwenye The Fresh Prince of Bel-Air.

Katika miaka ya 2000, Long alijiunga kama mshiriki wa igizo la Third Watch, ambapo alicheza kama ofisa wa NYPD Sasha Monroe. Mnamo mwaka 2024, ilitangazwa kuwa Long atacheza uhusika wa Katherine Jackson katika filamu ya wasifu ya Michael Jackson iitwayo Michael iliyotoka mwaka 2026.[4]

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]
MwakaJinaUhusikaMaelezo
1991Boyz n the HoodBrandi
1995FridayDebbie
1997Love JonesNina Mosley
1997Soul FoodRobyn "Bird" Joseph
1999The Best ManJordan Armstrong
2000Big Momma's HouseSherry Pierce
2005Are We There Yet?Suzanne Kingston
2023You PeopleFatima Mohammed
2026MichaelKatherine Jackson[5]

Televisheni

[hariri | hariri chanzo]
MwakaJinaUhusikaMaelezo
1991–1993Guiding LightKat SpeakesUhusika wa kudumu
1994–1995The Fresh Prince of Bel-AirLisa WilkesMsimu wa 5
2003–2005Third WatchSasha MonroeUhusika mkuu
2017EmpireGiuliana 'Giusi' GreenUhusika wa mara kwa mara
2017–2018NCIS: Los AngelesShay MosleyUhusika mkuu

Tuzo na teuzi

[hariri | hariri chanzo]

Long amepokea tuzo kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

  • **NAACP Image Awards:** Alishinda mara tatu (2000, 2004, 2005).
  • **Black Reel Awards:** Alishinda kama Mwigizaji Bora mwaka 2000.
  1. "'Soul Food' Turns 25: See The Film's Cast Then And Now". www.essence.com. Septemba 27, 2022. Iliwekwa mnamo 2022-09-27.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Cummings, Renée (Machi 9, 2012). "Talita Long, mother of actress Nia Long...". Sunday Express.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Nia Long". Empire online. Bauer Media Group. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. D'Alessandro, Anthony (Januari 30, 2024). "Michael Jackson Biopic 'Michael' Sets Nia Long As Matriarch Katherine Jackson". Deadline Hollywood.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Grobar, Matt (Oktoba 3, 2023). "Lionsgate's Michael Jackson Biopic 'Michael' To Be Released Internationally By Universal".{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]