Ni Mimi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ni Mimi
Ni Mimi Cover
Studio album ya II Proud
Imetolewa 1995
Aina Hip hop
Lebo Don Bosco
Mtayarishaji Hard Blasters Crew
Marlone Linje[1]
Wendo wa albamu za II Proud
Ni Mimi
(1995)
Ndani ya Bongo
(1996)


Ni Mimi, ni jina la albamu ya kwanza kutoka kwa msanii wa muziki wa hip hop wa Dar es Salaam, Tanzania maarufu kama II Proud. Albamu imetoka mwaka 1995 - ikiwa kama albamu ya kwanza ya rap iliyotungwa kwa Kiswahili kwa utunzi wa rapa mwenyewe bila kunakili nyimbo za nje wala kuimba Kiingereza. Kuanzia utayarishaji mpaka mashairi ni ubunifu kamili ya rap ya Kiswahili. Albamu ya kwanza ya Kiswahili (lakini midundo na melody ni ya nyimbo za nje - Marekani ilikuwa ya Saleh Jabri iliyotoka mwaka 1991). Albamu zingine zilikuja baadaye kama vile Kwanza Unit (1994), Mabishoo ya Contish kutoka Zanzibar (1993).

II Proud alikuja kivingine sana. Mwitiko kutoka kwa hadhira ulikuwa mkubwa sana ukapelekea kutoka albamu nyingine mwaka uliyofuata Ndani ya Bongo.

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya nyimbo katika albamu ya Ni Mimi':

Upande Jina la wimbo Maelezo
A1 Ni Mimi
A2 Yah Oh Yanatisha
A3 Blood Shed
A4 Kesho Kwa Mungu
A5 Instrument Midundo mitupu
A6 Siku (Original) Mkono wa HBC ndani ya Soundcrafters Studio
B1 Ni Wapi? Wimbo huu ndio uliotolewa kama singo na ulikuwa gumzo wakati huo.
B2 Siku (Ext. Version)
B3 Kama Hivi (Feat. Hardblasters)
B4 Ni Mimi (Bassmix)
B5 Shoutout

Kikosi kazi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Dar es Salaam Histories from an Emerging African Metropolic cha James R. Brennan, Andrew Burton na Yusuf Lawi

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]