Ngw'anamalundi (Mwanamalundi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Katika kigezo hiki unataja tarehe YYYY|MM|DD maana yake ni 1999|10|24 kwa maana "24 Oktoba 1999"


Igulu Bugomola
AmezaliwaMwakubunga Nera
AmefarikiMwanza
Majina mengineNgw'anamalundi
Kazi yakeMcheza ngoma za kisukuma

Ngw'anamalundi (kwa matamshi mengine Mwanamalundi) ni jina maarufu katika masimulizi ya kabila la Wasukuma. Alikuwa mcheza ngoma mashuhuri kutoka kabila hilo ambaye alipewa jina hilo kama utani likimaanisha miguu myembamba na mirefu [1]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Ngw'anamalundi alizaliwa katika kijiji cha Mwakubunga Nera katika Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza mnamo 1846[2] na kupewa jina la Igulu Bugomola, Igulu ikiwa na maana ya mbingu. Alizaliwa akiwa mtoto wa mwisho na wa pekee wa kiume kati ya watoto wanne wa familia ya mzee Bugomola na Ngolo Igulu.

Igulu (Ngw'anamalundi) alikua na tabia ya uzururaji na haikuwa rahisi kumkuta nyumbani. Alikua mahiri wa kucheza ngoma, na mara nyingi alifuatwa na kundi la watoto kwa sababu hiyo. Hali hii iliwachukiza wazazi wengi kutokana na kwamba watoto wao, ambao pia walikuwa wakiwategemea katika kuchunga mifugo, waliwatelekeza mifugo na kumfuata Igulu, hivyo kupelekea kupotea kwa watoto wa mifugo hao. Walimkebehi kwa msemo wa “Mamirundi galyo lilihumbura bhana bhise” ikiwa na maana ya “mamiguu yake marefu linarubuni watoto wetu”: hiyo ilipelekea kufutika jina la Igulu na kuwa Ng’anamalundi.

Maisha yake kama mcheza ngoma[hariri | hariri chanzo]

Ngw’anamalundi alianza kujiimarisha kwenye ngoma baada ya kuona watu wengi kijijini wanamchukia, huku kulimpelekea kuanza tena kupendwa na vijana wengi; alipata wafuasi kiasi kwamba alianza kutumika kama jeshi la kukodiwa na Watemi vinapotokea vita. Kikundi chake kilikua na kuanza kutumika katika sherehe mbalimbali kwenye familia za kitemi za wakati huo.

Mwanzo wa miujiza[hariri | hariri chanzo]

Siku moja Ngw’anamalundi na wenzake wawili walikwenda kwa bibi kizee mmoja kutafuta dawa, ili iwasaidie katika shughuli zao za ngoma; kizee huyo alipatikana katika msitu mkubwa na alikubali kuwasaidia.

‘’Tujagi lolo ngh’wiporu bhana bhane’’ akiwa na maana ya "twendeni sasa porini watoto wangu", bibi huyo aliwaambia Ngw’anamalundi na wenzake ili waongozane naye kwenda porini.

Njiani bibi alikamata vinyonga watatu na kuwawekea kichwani kila mmoja, kisha safari ikaendelea kuelekea katikati ya pori. Baada ya kufika katikati ya pori hilo nene, mzee aliwaambia wasimame na kuamuru kila mmoja achimbe shimo refu sawa na urefu wake mpaka kiunoni. Baada ya zoezi hilo kukamilika aliwaambia wakusanye kuni na kuzitumbukiza. Baada ya hapo waliwasha moto kwa njia ya kupekecha, moto ulipokolea sana waliwachukua wale vinyonga watatu na kuwawekea dawa midomoni mwao na kuwatupia ndani ya moto huo, wakateketea wote. Wakiwa wanaendelea kushangaa kuungua kwa vinyonga hao, Ngw’anamalundi na wenzake walimwona [kifaru]] akitoka kwenye moto huo na kuanza kuwakimbiza, wote walikimbia hovyo kila mmoja na njia yake.

Ngw’anamalundi alikimbia na kupanda juu ya mti, kifaru yule alifika kwenye shina la mti na kuanza kuliparua kwa hasira na baada ya muda aliondoka, Ngw’anamalundi alimwona bibi yule akikutana na kifaru kabla hata hajafika mbali, na alimshuhudia akimrarua bibi yule mpaka akafa.

Kifo chake[hariri | hariri chanzo]

Kaburi lake lipo Seke katika Mkoa wa Shinyanga likitembelewa na wafuasi wa dini za jadi.[3]

Kishosha Sitta, mjukuu wa Ngw'anamalundi, akiwa na umri wa miaka 78 alifanya mahojiano na gazeti la Mwananchi na kusimulia historia ya babu yake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [1], tovuti ya gazeti la Mwananchi, 18 Januari 201, iliangaliwa Desemba 2018
  2. Mningo 2015, uk. 50
  3. Joseph L. Mbele, Hero in Sukuma Prose Narratives, makala katika Peek-Yankah 2004

Vitabu[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ngw'anamalundi (Mwanamalundi) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.