Neymar Jr

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Neymar Jr akiwa Paris Saint Germain

Neymar da Silva Santos Júnior (matamshi ya Kireno: [nejˈmaʁ dɐ ˈsiwvɐ ˈsɐ̃tus ˈʒũɲoʁ], kwa kawaida anajulikana kama Neymar au Neymar Jr; amezaliwa 5 Februari 1992) ni mchezaji wa mpira wa miguu mzawa wa Brazil.

Ni mchezaji ambaye anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya Paris Saint-Germain nchini Ufaransa na timu ya taifa ya Brazil.

Neymar alijitokeza katika umri mdogo huko Santos, ambako alifanya mwanzo wake wa kitaaluma mwenye umri wa miaka 17. Na keymar alikuwa mara mbili mchezaji bora wa brazil mwaka 2011 na 2012, kabla ya kuhamia Ulaya kwendujiunga na Barcelona. Akiwa kama mshambuliaji akisaidiana na Lionel Messi na Luis Suárez, alishinda kombe la La Liga, Copa del Rey, na Ligi ya Mabingwa ya UEFA msimu wa 2014-15, . Alishika nafasi ya tatu katika tuzo ya Ballon d'Or mwaka 2015. Mnamo Agosti 2017, Neymar alihamia kutoka Barcelona kwenda Paris Saint-Germain kwa mkataba wa thamani ya milioni 222 milioni, na kumfanya awe mchezaji wa gharama kubwa duniani.


Pamoja na mabao 55 katika mechi 85 kwa Brazil tangu kuanzia umri wa miaka 18, Neymar ndiye mchezaji wa tatu wa juu zaidi kwa timu yake ya kitaifa. Ushiriki wake katika Kombe la Dunia ya FIFA ya 2014 na 2015 Copa América ilipunguzwa kwa kuumia na kusimamishwa kwa mtiririko huo, lakini mwaka ujao aliipatia Brazil medali ya kwanza ya dhahabu ya Olimpiki katika soka la wanaume katika michezo ya Olimpiki ya majira ya joto ya 2016.


Anajulikana kwa njia yake ya uwezo wa miguu miwili. Yeye huwa miongoni mwa watu wa michezo maarufu duniani;kampuni ya SportsPro ilimtaja Neymar kama mwanamichezo maarufu zaidi duniani mwaka 2012 na 2013, na ESPN imemtaja kuwa mwanariadha maarufu zaidi wa nne mwaka 2016.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Neymar Jr kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.