New Times LA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jiji la Los Angeles katika Jimbo la California.Katika jiji hili,gazeti la New Times LA lilichapishwa na kuuzwa.

New Times LA ni gazeti lakitambo lililokuwa likichapishwa kila wiki katika eneo la Los Angeles,California.Lilichapishwa na Shirika la New Times Media tangu mwaka wa 1996 hadi mwaka wa 2002. Mhariri mkuu wa muda wake wa kuchapishwa alikuwa Rick Barrs. Mwandishi Jill Stewart ndiye aliyekuwa anaandika makala ,yaliyoleta utata, ya kisiasa.

Katika mwaka wa 2002,New Times Media iliingia mkataba wa kutoshindana na shirika la Village Voice Media, shirika jingine cha uchapishaji magazeti ya kila wiki. Mkataba wao ulikuwa: kampuni hizo zingewacha kuchapisha magazeti ya New Times LA na Cleveland Free Times(gazeti la Village Voice Media) ili zisikuwe zikishindana katika mji wowote ule. Gazeti lililoshindana na New Times LA lilikuwa LA Weekly. New Times Media inaendelea kuchapisha majarida mengine mbalimbali kama Miami New Times,New Times Broward-Palm Beach na Phoenix New Times.

Mkataba huu ulifuatwa na upelelezi kutoka idara ya Haki ya Marekani. Uchunguzi ulisababisha malipo kutoka kampuni zote mbili,zikialazimishwa kuuza mali zao na magazeti yao ya kitambo kwa washindani wao.

Mali zao zilihusu vitu kama "samani ya ofisi, mifumo ya simu","haki zote za uchapishaji wa magazeti kwenye karatasi na pia ya kielektroniki", "leseni na vibali vya vituo vya usambazaji"na "orodha zote za wateja,mikataba,akaunti na rekodi za mikopo." [1]

Mali zote za New Times LA zilinunuliwa na kampuni ya Southland Publishing,Inc ambayo huchapisha magazeti kadhaa ya kila wiki ya mitaa. Kutoka kwa mali walizopata,Southland iliweza kuanzisha magazeti mawili: Los Angeles CityBeat na ValleyBeat. [2]

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]