Neema Mosha
| Neema Ramadhan Mosha | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Kazi yake | Mtaalamu wa Biostatistiki |
Neema Ramadhan Mosha (alizaliwa Tanzania, 17 Machi 1990) ni mtaalamu wa takwimu za kitabibu na wa biostatistiki, NA mtafiti wa afya ya umma kutoka Tanzania. Ana shahada ya uzamivu ya Epidemiolojia akibobea katika Biostatistiki kutoka Chuo Kikuu cha Stellenbosch, Afrika Kusini. Amefanya kazi katika tafiti za afya ya umma, majaribio ya kitabibu, utafiti wa utekelezaji, na tathmini za miradi ya afya kwa zaidi ya miaka 14.
Kwa sasa anafanya kazi kama Mshiriki wa Utafitikatika Mwanza Intervention Trials Unit (MITU)[1], Tanzania, na Chuo Kikuu cha Ludwig-Maximilians (LMU), Munich, Ujerumani. Pia ameshiriki kama mshauri wa takwimu kwa taasisi mbalimbali za kimataifa, zikiwemo UNICEF, Benki ya Duni, World Vision, War Child na Liverpool School of Tropical Medicine.
Maeneo yake ya utafiti yanajumuisha UKIMWI na magonjwa ya zinaa, magonjwa yasiyoambukiza, afya ya akili, lishe, ukatili wa kijinsia, afya ya watoto, afya ya wanawake, mifumo ya afya, pamoja na magonjwa yanayoibuka.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Alipata Shahada ya Sayansi katika Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma mwaka 2011. Baadaye alipata Shahada ya Uzamili katika Epidemiolojia na Biostatistiki kutoka Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMUCo) mwaka 2014, ambapo alifanya utafiti kuhusu kiwango cha shinikizo la damu na sababu zinazohusiana nacho kaskazini-magharibi mwa Tanzania.
Mwaka 2022 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Epidemiolojia, akibobea katika Biostatistiki, kutoka Chuo Kikuu cha Stellenbosch, Afrika Kusini. Tasnifu yake ilichunguza athari za upungufu wa taarifa katika makadirio ya maambukizi na kuenea kwa VVU katika tafiti za ufuatiliaji wa idadi ya watu.
Mbali na utafiti, Mosha amefundisha katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu, ikiwemo Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMC), Catholic University of Health and Allied Sciences (CUHAS), Ludwig-Maximilians University na London School of Hygiene & Tropical Medicine.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Neema Mosha amepokea tuzo na ufadhili mbalimbali wa kitaaluma kutokana na mafanikio yake katika elimu na utafiti.
Mwaka 2019, alitambuliwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wa Tanzania wanaotoa mfano kwa kizazi cha vijana kupitia mradi wa TanzaniasHeroes2019[2]. Utambuzi huo ulitolewa kupitia kitabu kilichochapishwa kwa ushirikiano kati ya Launchpad na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania.
Mosha ameeleza kuwa moja ya mafanikio yake makubwa ni kukamilisha Shahada ya Uzamivu katika taaluma ya biostatistiki, ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikitawaliwa na wanaume.
Neema Mosha ametambuliwa kitaaluma kupitia nafasi mbalimbali za uongozi na ushiriki katika mashirika ya kitaaluma. Ni msemaji wa Tanzania katika International Biometrics Society (IBS) na pia ni mshiriki wa MRC Statistics and Epidemiological Partnership (ISEP), mpango unaolenga kujenga uwezo wa wataalamu wa biostatistiki barani Afrika.
Machapisho
[hariri | hariri chanzo]Neema Mosha ameandika na kushiriki kuandika machapisho [3] mengi ya kisayansi yaliyohakikiwa na wataalamu, hasa katika nyanja za epidemiolojia, biostatistiki na afya ya umma. Baadhi ya machapisho yake ni:
- Experience of physical violence during pregnancy and its association with behavioral outcomes during the prenatal and postnatal period: a pooled analysis of cross-sectional data from 45 low-income and middle-income (2025)
- Caregiver characteristics and behaviours: quantitative associations with child depression amongst refugees in Uganda. (2025)
- Longitudinal record linkage in sub-Saharan Africa countries: recommendations for healthcare research.(2024)
- Women's informal group participation and intimate partner violence in Mwanza, Tanzania (2024)
- The Association Between Depression, Suicidal Thoughts and Intimate Partner Violence Perpetration Among Young Men in Mwanza, Tanzania (2024)
- Exposure to pornographic material and perpetration of intimate partner violence among young men in Mwanza Tanzania.(2024)
- The association between alcohol consumption and intimate partner violence in young male perpetrators in Mwanza,Tanzania (2023)
- The short and long-term impact of COVID-19 restrictions on women’s mental health in Mwanza, Tanzania (2023)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu wasifu wa Mtanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |