Ndutu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Tembo akiwa karibu na eneo la Ndutu

Ndutu ni eneo lililo katikati kusini mwa Serengeti na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro katika mkoa wa Arusha nchini Tanzania.

Ndutu ni eneo zuri la kutembelea hasa kati ya mwezi Desemba na mwanzoni mwa mwezi Aprili ambapo makundi mengi ya wanyama wanaokula nyasi pamoja na pundamilia wanajazana katika eneo hili kwa ajili ya kuzaliana (kuzaa). Maficho ya wanyama hawa katika eneo hili imerekodiwa kuanza Januari hadi katikati ya mwezi Machi ambapo zaidi ya asilimia 80 ya wanyama wanaanza kuzaa wiki chache baadaye.

Licha ya kujificha, pia makundi makubwa ya wanyama hawa huenda katika eneo la Ndutu kwa ajili ya kujipatia chakula kutokana na uwingi wa nyasi zinazokuwa zimestawi kutokana na mvua.

Hata hivyo uwepo wa wanyama hao katika eneo hili una wavutia wanyama wakali kama simba, chui na fisi kwa ajili ya mawindo ili kujipatia chakula.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania (Tanzania the land of Kilimanjaro, Zanzibar and Serengeti)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Safiri Tanzania Utalii wa Tanzania

WikiLettreMini.svg Makala hii kuhusu "Ndutu" ni fupi mno. Inahitaji kupanuliwa mapema.
Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ndutu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.