Nenda kwa yaliyomo

Ndugu Wadogo Wamisionari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ndugu Wadogo Wamisionari (kwa Kireno: Frades Menores Missionários; kwa Kilatini: Fratres Minores Missionarii; kifupi: F.M.M.) ni watawa wanaume Wafransisko wa Kanisa Katoliki wenye makao makuu huko Ponta Grossa, Paraná (Brazil).

La kwao ni shirika la maisha yaliyowekwa wakfu kwa Mungu kwa njia ya nadhiri ya kushika mashauri ya Kiinjili ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu kadiri ya Kanuni ya Ndugu Wadogo na karama nzima ya mtakatifu Fransisko wa Asizi.

Uundaji na ustawi

[hariri | hariri chanzo]

Jumuia yao ilianzishwa na Wakapuchini waliotoka shirika lao. Tarehe 15 Agosti 1973 waLIkubaliwa rasmi na askofu Geraldo Micheletto Pellanda, C.P., wa Ponta Grossa kwa jina la Mapadri wa Mt. Fransisko wa Asizi, ila miaka 7 baadaye ikapewa jina la sasa. Chama hicho kikawa shirika la kijimbo kwa hati ya askofu huyohuyo ya tarehe 30 Mei 1982.

Wenye nadhiri ni 50 hivi katika konventi na parokia 8 nchini Brazil.

Tangu tarehe 15 Agosti 2017 kuna tawi la wanawake pia: Dada Wafransisko Wadogo Wamisionari (Irmãs Franciscanas Menores Missionárias).

    Viungo vya nje

    [hariri | hariri chanzo]
    Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
    Je, unajua kitu kuhusu Ndugu Wadogo Wamisionari kama historia yake au maelezo zaidi?
    Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
    Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.