Ndola (Ileje)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Ndola
Nchi Tanzania
Mkoa Mkoa wa Songwe
Wilaya Ileje
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 6,741

Ndola ni kata ya Wilaya ya Ileje katika Mkoa wa Songwe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 53403.

Kata hiyo ina vijiji 4: Igumila, Ibezya, Ndola na Ishenta. Makao makuu ya kata yapo Ndola, ambapo ni katikati ya vijiji vyote vinne. Ofisi za kata zinapatikana pale Ndola, ambapo kuna ofisi za Diwani, Afisa Mtendaji Kata, Afisa Elimu Kata, Afisa Kilimo na Afisa Ugani.

Kijiji cha Ndola kina jumla ya vitongoji saba ambavyo ni: Isanga, Ndola, Isagama, Kaloleni, Tunduma, Kaburu na Ileya.

Ishenta ina vitongoji kama Itula, Selenje, Mdibe na Ibututu.

Igumila ina vitongoji vitatu: Mpiru, Ilembo na Igumila.

Ibezya ina vitongoji kama Ilulu, Ulando, Ibezya.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 6,741 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,820 [2] walioishi humo.

Kuhusu huduma za afya, kata ya Ndola ina Kituo cha Afya cha Ndola (Ndola Health Center); kituo hicho kipo makao makuu ya kata, Ndola. Pia kata ina zahanati ya Ishenta (Ishenta dispensary) ambayo ipo kijiji cha Ishenta na Zahanati ya Ibezya ambayo ipo kijiji cha Ibezya na imejengwa na kufunguliwa mwaka 2024. Katika kijiji cha Igumila wananchi kwa kushirikiana na serikali ya kata wameanza ujenzi wa zahanati.

Kata ya Ndola ina jumla ya shule za msingi tano ambazo ni: Shule ya Msingi Ndola, Shule ya Msingi Ibezya, Shule ya Msingi Ileya, Shule ya Msingi Igumila na Shule ya Msingi Ishenta.

Kata ina Shule ya Sekondari Ndola ambayo ipo karibu na Kituo cha Afya Ndola, katika makao makuu ya kata.

Kata ya Ndola ina vyanzo mbalimbali vya maji kama vile mto Iyela ambao ni chanzo cha maji ya Itumba na Isongole, makao makuu ya wilaya.

Kata ya Ndola ina jumuiya ya wananchi wanaotumia maji inayoitwa UMOJA, ambayo Ofisi zake zinapatikana makao makuu ya kata Ndola; inajumuisha wanufaika wa maji katika vijiji vya Ishenta, Ndola, Igumila, Ishinga, Yenzebwe na Ibezya.

Mazao yanayopatikana katika kata ya Ndola ni pamoja na karanga, mahindi, ulezi, viazi vitamu (mbatata), viazi mviringo, alizeti, soya, parachichi, kahawa n.k.

Kuna soko la mifugo la Ikwesela ambalo lipo kila Jumanne kijiji cha Ishenta.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz, uk 235
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Ileje DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-03-13. 
Kata za Wilaya ya Ileje - Mkoa wa Songwe - Tanzania

Bupigu | Chitete | Ibaba | Ikinga | Isongole | Itale | Itumba | Kafule | Kalembo | Lubanda | Luswisi | Malangali | Mbebe | Mlale | Ndola | Ngulilo | Ngulugulu | Sange |


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Songwe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ndola (Ileje) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .
Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno