Ndizi sukari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkungu wa ndizi sukari.
Ndizi sukari.

Ndizi sukari ni tunda lenye rangi ya njano ambalo huliwa na viumbe hai, kwa mfano watu, nyani, tembo na wengine wengi. Tunda hili linapendwa sana kwa sababu lina ladha tamu ya sukari iliyo ya asili na ambayo hujenga miili ya viumbe hai.

Kwa watu tunda hili lina faida nyingi: mojawapo ni kwamba huwapatia vitamini C mwilini na kuwafanya kuwa na afya bora.

Tunda hili hustawi sana katika maeneo yenye joto la kawaida, kwani joto huchangia kuiva kwa tunda hili: ndio maana tunda hili hustawi na kupatikana sana barani Afrika kwa sababu kuna joto la kawaida linalosaidia ukuaji wa tunda hili.

Mti wa ndizi sukari huitwa mgomba ambao humwagiliwa maji ya kawaida au maji ya sabuni na kustawi tofauti na miti mingine ambayo ikimwagiwa maji ya sabuni hupoteza uhai.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndizi sukari kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.