Ndege wa Zimbabwe
Mandhari

Ndege wa Zimbabwe aliyechongwa katika mawe ni nembo ya taifa ya Zimbabwe, inayoonekana kwenye bendera na ngao za taifa za Zimbabwe na iliyokuwa Rhodesia, pamoja na kwenye noti na sarafu (kwanza kwenye Rhodesian pound kisha kwenye Rhodesian dollar). Inaaminika kuwa inawakilisha tai aina ya bateleur (Terathopius ecaudatus) au tai maji wa Afrika (Haliaeetus vocifer).[1][2] Muundo wa ndege huyo unatokana na idadi ya sanamu zilizochongwa kwa jiwe la sabuni (soapstone) zilizopatikana katika magofu ya mji wa zamani wa Zimbabwe Kuu.
Sasa hivi ndicho kielelezo cha kudumu cha Zimbabwe huru, na mtaalamu wa akiolojia Edward Matenga aliorodhesha zaidi ya mashirika 100 ambayo sasa yanajumuisha ndege huyo kwenye nembo zao.[3][4][5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Thomas N. Huffman (1985). "The Soapstone Birds from Great Zimbabwe". African Arts. 18 (3): 68–73, 99–100. doi:10.2307/3336358. JSTOR 3336358.
- ↑ Paul Sinclair (2001). "Review: The Soapstone Birds of Great Zimbabwe Symbols of a Nation by Edward Matenga". The South African Archaeological Bulletin. 56 (173/174): 105–106. doi:10.2307/3889033. JSTOR 3889033.
- ↑ Edward Matenga (2001). "The Soapstone Birds of Great Zimbabwe". Studies in Global Archaeology. 16: 1–261.
- ↑ Great Zimbabwe (11th–15th century) | Thematic Essay | Timeline of Art History | The Metropolitan Museum of Art
- ↑ Hall, Martin; Stefoff, Rebecca (2006). Great Zimbabwe. Oxford University Press, USA. uk. 30. ISBN 978-0-19-515773-4.
| Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |