Nchi ya Moto

Majiranukta: 54°S 70°W / 54°S 70°W / -54; -70
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tierra de Fuego - Nchi ya Moto.
Bandari ndogo ya Porto Williams upande wa Chile.

Nchi ya Moto (ndiyo tafsiri ya jina Tierra del Fuego) ambayo ni funguvisiwa kwenye kusini kabisa ya Amerika Kusini. Imetengwa na bara kwa Mlangobahari wa Magellan. Rasi ya Hoorn ambayo ni ncha ya kusini kabisa ya Amerika, iko hapa.

Visiwa vyote vina eneo la kilomita za mraba 73,746 na kisiwa kikuu Isla Grande de Tierra del Fuego kina km2 47.000.

Tangu mwaka 1881 funguvisiwa limegawiwa kwenye longitudo ya magharibi ya 69° 31' kwa nchi mbili za Chile na Argentina. Upande wa mashariki, katika mkoa wa "Tierra del Fuego", kuna wakazi wapatao 127.000, upande wa magharibi, katika mkoa wa Magellanes wa Chile, kuna watu 8,000.

Jina linatokana na kumbukumbu ya wapelelezi Wahispania waliovuka Amerika Kusini kwenye mwaka 1520. Walipopita hapa hawakuona watu wowote lakini wakati wa usiku waliona mioto mingi, hivyo Magellan aliandika "Nchi ya moto" katika ramani yake.

Hata baada ya kuanzishwa kwa ukoloni wa Hispania katika sehemu za kaskazini ya Amerika Kusini, wenyeji Waindio, waliokuwa wavuvi na wawindaji, waliendelea kuishi tu bila usumbufu kwa muda mrefu hadi karne ya 19.

Kuanzia mwaka 1860 wafugaji wa kondoo kutoka Argentina na wachimbaji madini kutoka Chile walianza kuingia kwenye Tierra del Fuego. Pamoja na kunyang'anywa ardhi yao wazalendo wengi walikufa baada ya kuambukizwa magonjwa kutoka Ulaya ambayo hawakuzoea, sawa jinsi ilivyowahi kutokea kwa Waindio wengi tangu kuingia kwa Wazungu. Leo ni wachache sana waliobaki.

Eneo ni baridi mno kwa kilimo lakini hadi leo ufugaji wa kondoo na biashara ya sufi ni msingi wa uchumi. Kampuni ya nguo Bennetton inamiliki maeneo ya kilomita za mraba milioni moja kwa ufugaji wa kondoo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

  • Bridges, Lucas. 1948. Uttermost Part of the Earth. Reprint with introduction by Gavin Young, Century Hutchinson, 1987. ISBN|-7126-1493-1
  • Keynes, Richard. 2002. Fossils, Finches and Fuegians: Charles Darwin's Adventures and Discoveries on the Beagle, 1832–1836. HarperCollins Publishers, London. Reprint: 2003.
  • Bollen, Patrick. 2000. "Tierra del Fuego" B/W Photobook. Lannoo Publishers, Tielt, Belgium. ISBN 90-209-4040-6
  • Pisano Valdés, E. (1977). "Fitogeografía de Fuego-Patagonia chilena. I.-Comunidades vegetales entre las latitudes 52 y 56º S". Anales del Instituto de la Patagonia (kwa Spanish) VIII. Punta Arenas. 

Tovuti za Nje[hariri | hariri chanzo]

Tierra del Fuego travel guide kutoka Wikisafiri

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

54°S 70°W / 54°S 70°W / -54; -70