Nathan Méténier
Nathan Méténier (alizaliwa Juni 1999) ni mwanaharakati wa hali ya hewa na mazingira nchini Ufaransa. Alikuwa mmoja wa wanachama wachanga zaidi wa Kikundi cha kwanza cha Ushauri cha Vijana cha Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi kutoka mwaka 2020 hadi 2022.[1][2][3][4][5][6]
Ndiye mwanzilishi wa Generation Climate Europe,[7] muungano mkubwa zaidi wa mitandao inayoongozwa na vijana katika ngazi za Ulaya, ikisukuma hatua kali kutoka kwa Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya hali ya hewa na mazingira.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Nathan Méténier alikulia mjini Grenoble,[8] katika Milima ya Alps nchini Ufaransa ambapo aliweza kushuhudia athari za mabadiliko ya tabianchi kwa macho yake mwenyewe. Alitangaza: “Nimeona mabadiliko, nimeona barafu ikitoweka na kuporomoka kwa mlima Mont Blanc”[7]
Amefanya kazi na kushiriki katika mashirika na harakati nyingi haswa kama Mkurugenzi wa Kanda wa Youth4Nature na msemaji wa Vijana na Mazingira barani Ulaya. Alihitimu kutoka Taasisi ya Grenoble ya Mafunzo ya Siasa. Na kwa sasa anasomea katika Chuo cha London School of Economics.[9][10]
Kuanzia mwaka 2019 hadi 2021, Méténier alikuwa mjumbe kwenye Bodi ya Vijana na Mazingira barani Ulaya. Yeye ni mwanzilishi na mratibu wa Generation Climate Europe, na pia Yeye ni balozi wa Youth4Nature.[9][11] Yeye ndiye mwanzilishi wa Generation Climate Europe ambao muungano mkubwa zaidi wa mitandao inayoongozwa na vijana katika ngazi za Ulaya, akisukuma hatua madhubuti kutoka kwa Umoja wa ulaya juu ya masuala ya hali ya hewa na mazingira.
Mnamo mwezi Julai mwaka 2020 hadi 2022, Méténier aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeitwa António Guterres kwa mara ya kwanza katika Kikundi cha Ushauri cha Vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi kilicho na viongozi saba wa vijana wa hali ya hewa kuweza kumshauri kuhusu hatua za kukabiliana na mgogoro wa hali ya hewa kwa kipindi cha miaka miwili.[12][13] Méténier alikuwa mmoja wa vijana walio na umri wa kati ya miaka 18 hadi 28. Alikuwa pekee aliyewakilisha nchi ya Ufaransa na Ulaya ya Magharibi.[12]
Harakati
[hariri | hariri chanzo]Méténier amelenga hasa kuimarisha sauti ya harakati za vijana huko mjini Brussels.[1][3] Alianzisha Generation Climate Europe mwaka wa 2019 akiwa na nia ya kukusanya vuguvugu kuu la vijana barani Ulaya linalohusika na masuala ya mazingira.[10]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 www.euronews.com https://www.euronews.com/green/2020/10/19/the-un-s-21-year-old-climate-advisor-who-is-nathan-metenier. Iliwekwa mnamo 2025-10-20.
{{cite web}}: Missing or empty|title=(help) - ↑ United Nations. "The Youth Advisory Group on Climate Change". United Nations (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-20.
- 1 2 Nathan Méténier, le militant écolo devenu jeune conseiller climat auprès de l’ONU (kwa Kifaransa), 2021-01-05, iliwekwa mnamo 2025-10-20
- ↑ "UK's oil consultant contract for climate talks sparks concern". France 24 (kwa Kiingereza). 2021-03-10. Iliwekwa mnamo 2025-10-20.
- ↑ Dali ten Hove (2020-12-11). "Meet the 20-Somethings Advising the UN Chief on How to Save Planet Earth - PassBlue". passblue.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-10-20.
- ↑ Christelle Ibach, Rédactrice pour Cadre Dirigeant Magazine Strasbourg (2020-09-29). "Nathan Méténier, conseiller climat pour l'ONU". Cadre & Dirigeant Magazine (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2025-10-20.
- 1 2 www.euronews.com https://www.euronews.com/green/2020/10/19/the-un-s-21-year-old-climate-advisor-who-is-nathan-metenier. Iliwekwa mnamo 2025-10-20.
{{cite web}}: Missing or empty|title=(help) - ↑ Ville de Grenoble. "Nathan Méténier : cap vert - Transitions". www.grenoble.fr (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2025-10-20.
- 1 2 "Nathan Méténier - Advocacy Manager ⋆ YEE", YEE (kwa American English), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-30, iliwekwa mnamo 2025-10-20
- 1 2 Léna Guihéneuf (2020-09-21). "Nathan Méténier, étudiant londonien et conseiller climat auprès de l'ONU". French Morning London (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2025-10-20.
- ↑ "Nathan — Youth4Nature". Youth4Nature (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-30. Iliwekwa mnamo 2025-10-20.
- 1 2 Vesna Blazhevska (2020-07-27). "Young leaders tapped to invigorate UN's climate action plans, hold leaders to account". United Nations Sustainable Development (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-10-20.
- ↑ United Nations. "The Youth Advisory Group on Climate Change - 2020". United Nations (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-20.