Natasha Thahane
Nokuthula Natasha Thahane Tutu (alizaliwa 25 Septemba, 1995) ni mwigizaji, mwanamitindo, na mtu mashuhuri wa vyombo vya habari kutoka nchini Afrika Kusini.
Anajulikana zaidi kwa nafasi zake katika mfululizo wa vipindi vya televisheni kama Blood & Water, Skeem Saam, The Queen, na It's OK We're Family. Hivi karibuni, alijiunga na drama ya BET, Isono, akicheza nafasi ya Millicent.[1]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Thahane alizaliwa Orlando East kwa wazazi Trevor Thamsanqa Tutu na Nomaswazi Mamakoko. Yeye ni mjukuu wa Askofu Mkuu Desmond Tutu. Baadae alihamia Cape Town, ambapo alisoma katika Shule ya Sekondari ya Milnerton.
Baada ya hapo, alihitimu shahada ya uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Witwatersrand. Mwaka 2018, alikamilisha mpango wa mwaka mmoja wa mafunzo ya uigizaji wa filamu katika New York Film Academy, Manhattan.[2][3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Magadla, Mahlohonolo. "Style Crush: Natasha Thahane". Truelove (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-10-30.
- ↑ Ndlangisa, Amanda (29 Agosti 2016). "Celebs supporting Stop Racism Pretoria Girls High". Truelove (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-10-30.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Leteba, Lineo. "One on one with Natasha Thahane". Truelove (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-10-30.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Natasha Thahane kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |