Nanjala Nyabola
Nanjala Nyabola ni mwandishi wa Kenya, mchambuzi wa siasa na mwanaharakati anayeishi Nairobi, Kenya.[1]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Nyabola huandika kwa upana kuhusu jamii na siasa za Afrika, teknolojia, sheria ya kimataifa na masuala ya usawa wa kijinsia. Kitabu chake cha kwanza Digital Democracy, Analogue Politics: How the Internet Era is Transforming Kenya (kilichochapishwa na Zed Book mwaka 2018) kilisifiwa kuwa ni “lazima kusomwa” kwa watafiti na wanahabari wanaoandika kuhusu Kenya ya sasa.[2]
Nyabola alipokea ufadhili wa masomo wa Rhodes Scholarship katika Harris Manchester College, University of Oxford mwaka 2009. Pia alikuwa sehemu ya kundi la kwanza la washiriki wa Foreign Policy Interrupted mwaka 2017, na mshiriki wa mpango wa Logan Nonfiction katika Carey Institute for Global Good.
Aidha, ni mjumbe wa bodi ya Amnesty International Kenya.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Nyabola ana shahada kadhaa katika masuala ya siasa na sheria:
- Shahada ya kwanza (BA) katika Masomo ya Afrika na Sayansi ya Siasa, *University of Birmingham
- Shahada ya uzamili (MSc) katika Forced Migration, Chuo Kikuu cha Oxford
- Shahada ya uzamili (MSc) katika Masomo ya Afrika, Chuo Kikuu cha Oxford
- Shahada ya sheria (J.D.), Harvard Law School
Masomo ya kubadilishana katika Geneva Graduate Institute
Uandishi wa habari
[hariri | hariri chanzo]Nyabola ameandika sana kuhusu siasa za Afrika, hasa Kenya, pamoja na teknolojia, sheria ya kimataifa na masuala ya kijinsia. Makala zake zimechapishwa katika vyombo mbalimbali kama African Arguments, Al Jazeera, Financial Times, Foreign Affairs, Foreign Policy (magazine)|Foreign Policy, The Guardian, New African na vingine.
Makala yake ya mwaka 2014 katika Al Jazeera yenye kichwa “Why do Western media get Africa wrong?” ilisababisha mjadala mkubwa kimataifa, ikiwa ni pamoja na kujadiliwa katika BBC World Service.
Hotuba za umma
[hariri | hariri chanzo]Nyabola ni mzungumzaji wa mara kwa mara katika majukwaa ya kimataifa na vyuo vikuu kama University of Edinburgh, SOAS, University of London na Stanford University. Pia ameshiriki katika mikutano mbalimbali ya kimataifa kuhusu teknolojia na siasa, ikiwemo re:publica na RightsCon.
Machapisho
[hariri | hariri chanzo]Vitabu
[hariri | hariri chanzo]2020: Travelling While Black: Essays Inspired by a Life on the Move – mkusanyiko wa insha zinazochambua uzoefu wa kusafiri kama mwanamke Mwafrika Mweusi. 2018: Digital Democracy, Analogue Politics: How the Internet Era is Transforming Kenya 2018: Where Women Are: Gender & The 2017 Kenyan Elections (amehariri pamoja na wengine) 2022: Strange and Difficult Times: Notes on a Global Pandemic – insha kuhusu janga la COVID-19 na athari zake duniani
Sura za vitabu
[hariri | hariri chanzo]“Testimony as Text: Performative Vulnerability and the Limits of Legalistic Approaches to Refugee Protection” katika African Women Under Fire “Media Perspectives: Social Media and New Narratives: Kenyans Tweet Back”
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Prize Students Step-up to Receive Awards". University of Birmingham. 12 Julai 2008. Iliwekwa mnamo 1 Septemba 2020.
{{cite web}}: line feed character in|title=at position 6 (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Book Review: Digital Democracy, Analogue Politics: How the Internet Era is Transforming Kenya by Nanjala Nyabola". LSE Review of Books. 2018-12-07. Iliwekwa mnamo 2019-07-10.
{{cite web}}: line feed character in|title=at position 5 (help)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nanjala Nyabola kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |