Namanga, Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Namanga ni mji ambao uko kusini mwa Kenya, kwenye kaunti ya Kajiado mpakani mwa Tanzania.

Kulingana na sensa ya mwaka 1999 mji huu una watu 5,500 [1].

Mji huu upo kilomita 200 kutoka Nairobi na kilomita 130 kutoka mji wa Arusha (Tanzania).

Uchumi wa mji huu unategemea sana utalii. Watalii wengi wanaotembelea wanyama wa Hifadhi ya Taifa ya Amboseli hupitia kwenye mji huu.

Mlima Kilimanjaro unaonekana kusini mwa mji huu. Pia mlima Oldoinyo Orok uko kaskazini magharibi kwa mji huu na hujulikana kama milima ya Namanga.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Majiranukta kwenye ramani: 2°33′S 36°47′E / 2.55°S 36.783°E / -2.55; 36.783