Nenda kwa yaliyomo

Nafasiwakati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Katika fizikia, nafasiwakati, ni kielelezo cha hisabati ambacho huunganisha pandeolwa tatu za nafasi pamoja na pandeolwa moja ya wakati katika mfumo mmoja wa pandeolwa nne. Michoro ya nafasiwakati ni muhimu kwa kupiga picha akilini athari za uhusianifu, kama vile jinsi waangalizi tofauti ambavyo hutambua wapi na lini matukio yanatokea.

Hadi mwanzoni mwa karne ya 20, dhana ya kawaida ilikuwa kwamba jiometri yenye pandeolwa tatu ya ulimwengu (maelezo yake kulingana na mahali, maumbo, umbali, na maelekezo) ilikuwa tofauti kabisa na wakati. Hata hivyo, nafasi na wakati zilichukua maana mpya baada ya ugunduzi wa mgeuzo wa Lorentz na nadharia ya uhusianifu maalumu.

Mnamo 1908, Hermann Minkowski alitoa fasiri ya kijiometri ya uhusianifu maalumu ambayo iliunganisha wakati na pandeolwa tatu za nafasi katika mfumo mmoja wa pandeolwa nne ambao sasa unajulikana kama nafasi ya Minkowski. Fasiri hiyo ilitokea kuwa muhimu sana kwa nadharia ya uhusianifu wa jumla, ambapo nafasi na wakati hupindwa na tungamo na nishati.

Umakanika kawaida usio wa uhusianifu huchukulia wakati kama kipimo ambacho ni sare kokote ulimwenguni, ni tofauti na nafasi, na kinakubaliwa na waangalizi wote. Umakanika kawaida huchukulia kuwa wakati hupita bila kubadilika, bila kutegemea hali ya mwendo wa mwangalizi, au chochote cha nje.[1] Inadhania kwamba nafasi ni ile ya Euklides; yaani nafasi hufuata maarifa ya kawaida.[2]

Katika uhusianifu maalumu, wakati hauwezi kutengana na pandeolwa tatu za nafasi, kwa sababu kiasi ambavyo wakati hupita kwa mujibu wa kitu fulani kinaitegemea kasi ya kitu hicho kwa mujibu wa mwangalizi.[3] : 214–217 Uhusianifu wa jumla hutoa maelezo ya jinsi nyuga za uvutano zinavyoweza kupunguza kupita kwa wakati kwa mujibu kitu fulani kama inavyoonekana na mwangalizi nje ya uga.

  1. Rynasiewicz, Robert (12 Agosti 2004). "Newton's Views on Space, Time, and Motion". Stanford Encyclopedia of Philosophy. Metaphysics Research Lab, Stanford University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Julai 2012. Iliwekwa mnamo 24 Machi 2017.
  2. Davis, Philip J. (2006). Mathematics & Common Sense: A Case of Creative Tension. Wellesley, Massachusetts: A.K. Peters. uk. 86. ISBN 978-1-4398-6432-6.
  3. Schutz, Bernard (2004). Gravity from the Ground Up: An Introductory Guide to Gravity and General Relativity (kwa Kiingereza) (tol. la Reprint). Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 0-521-45506-5. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Januari 2023. Iliwekwa mnamo 24 Mei 2017.
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nafasiwakati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.