Nenda kwa yaliyomo

Nafasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfumo majiranukta Kartesi mwenye pandeolwa tatu unaotumiwa ili kuonyesha mahali katika nafasi

Nafasi ni mfumo wenye pandeolwa tatu ambao una mahali na mielekeo.[1] Kwa lugha ya kawaida, ni mahali patupu ambapo vitu vinaweza kuwekwa.[2] Katika fizikia kawaida, nafasi mara nyingi hutungwa kama pandeolwa tatu mstari. Wanafizikia wa kisasa kwa kawaida huichukulia, pamoja na wakati, kuwa sehemu ya mfumo wenye pandeolwa nne za nafasiwakati zisizo na kikomo.[3] Dhana ya nafasi ni muhimu kabisa katika kuelewa misingi ya ulimwengu. Hata hivyo, kutokubaliana kunaendelea kati ya wanafalsafa kuhusu kama nafasi ni halisi au sehemu ya mfumo wa dhana tu.

Katika karne za 19 na 20 wanahisabati walianza kuchungua jiometri ambazo si za Euklides, ambapo nafasi ni kama mchirizo, badala ya kuwa bapa kama katika nafasi ya Euklides. Kwa mujibu wa nadharia ya uhusianifu wa jumla ya Albert Einstein, nafasi karibu na nyuga za uvutano huachana na nafasi ya Euklides.[4] Lakini kwa kiwango kikubwa msongamano wa maada ni takriban sawa kokote ulimwenguni na hivyo ulimwengu ni takriban ya Euklides.[5]

  1. "Space – Physics and Metaphysics". Encyclopædia Britannica. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Mei 2008. Iliwekwa mnamo 28 Aprili 2008.
  2. TUKI. Kamusi ya Kiswahili Sanifu (tol. la 4). uk. 473.
  3. Bunyadzade, Konul (2018-03-15). "Thoughts of Time" (PDF). Metafizika Journal (kwa Kiazerbaijani). 1. AcademyGate Publishing: 8–29. doi:10.33864/MTFZK.2019.0. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 5 Aprili 2019. Iliwekwa mnamo 2018-03-15.
  4. Carnap, R. (1995). An Introduction to the Philosophy of Science. New York: Dove. (Original edition: Philosophical Foundations of Physics. New York: Basic books, 1966).
  5. NASA/WMAP Science Team (20 Februari 2024). "Will the Universe expand forever?" (kwa Kiingereza). National Aeronautics and Space Administration.
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nafasi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.