Nadiya Savchenko

Nadiya Viktorivna Savchenko (alizaliwa 11 Mei, 1981) ni mwanasiasa wa Ukraine, aliyewahi kuwa rubani wa usalama wa anga wa kijeshi katika Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine, na pia Naibu wa Watu wa Ukraine wa zamani.
Wakati wa Vita vya Donbas (2014–2022), Savchenko alikuwa luteni wa kwanza katika Jeshi la Nchi Kavu la Ukraine na alihudumu kama mwalimu wa kikosi cha kujitolea cha askari wa miguu, Kikosi cha Aidar. Mnamo Juni 2014, alikamatwa na vikosi vinavyoiunga mkono Urusi mashariki mwa Ukrainena kukabidhiwa kwa Urusi ambako alishtakiwa kwa kuongoza mashambulizi ya mizinga yaliyopelekea Kifo cha Igor Kornelyuk na Anton Voloshin nchini Ukraine.[1]
Baadaye alishtakiwa na kuhukumiwa kwa kosa la mauaji na kuvuka kinyume cha sheria mpaka wa taifa la Urusi, licha ya kuwa alikuwa tayari ametekwa kutoka katika ardhi ya Ukraine saa moja kabla ya vifo vya waandishi hao wa habari. Mmoja wa Wakili wake, Mark Feygin, alisema kuwa yeye alikuwa mfungwa wa vita na akazitaka Kamati ya Kimataifa za Msalaba Mwekundu na Umoja wa Mataifa kudai aachiliwe mara moja pamoja na wafungwa wengine wa vita vya Ukraine, la sivyo Urusi ichukuliwe kuwa imekiuka Mikataba ya Geneva. Mawaziri wa Umoja wa Ulaya na wawakilishi wao waliona kuwa kuzuiliwa kwake kulikuwa kinyume cha sheria na kwamba kesi yake haikuziheshimu haki za msingi za binadamu, ikiwemo haki ya mashauri.
Maisha na taaluma ya kijeshi
[hariri | hariri chanzo]
Nadiya Savchenko na dada yake mdogo Vira walizaliwa huko Kyiv katika kitongoji cha Troieshchyna.Baba yao alikuwa mhandisi wa kilimo, mama yao alikuwa mbunifu na msimamizi wa mizigo. Baba wa Savchenko alikuwa mwanachama wa Chama cha Kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti huku mama yake akiwa mwanaharakati wa kupinga Ukomunisti. Mama yake na dada yake Vira walisema kwenye mahojiano kwamba yeye na dada yake walilelewa katika nyumba inayozungumza Kiucrania na walihudhuria shule zinazofundisha kwa lugha ya Kiucrania.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ According to version by the prosecution, the rebels who captured Savchenko let her go and she crossed Russian border, "I have right for everything", by Novaya gazeta
- ↑ Why Russia needs the Ukrainian 'G.I. Jane' Savchenko imprisoned
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nadiya Savchenko kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |