Nenda kwa yaliyomo

Nadia Murad

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nadia Murad Basee Taha (alizaliwa 10 Machi, 1993) ni mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka nchini Iraq ambaye kwa sasa anaishi nchini Ujerumani [1] [2] Mnamo 2014, wakati wa mauaji ya kimbari ya Yazidi na Dola la Kiislamu, alitekwa nyara kutoka mji wake wa Kocho nchini Iraq. Sehemu kubwa ya jamii yake waliuwawa. Baada ya kupoteza sehemu kubwa ya familia yake, Murad alishikiliwa kama mtumwa wa ngono wa Dola ya Kiislamu kwa miezi mitatu, pamoja na maelfu ya wanawake na wasichana wengine wa Yazidi.

Murad ndiye mwanzilishi wa Nadia's Initiative, shirika lisilo la faida lililojitolea "kusaidia wanawake na watoto walioathiriw na mauaji ya kimbari, ukatili mkubwa, na biashara haramu ya binadamu ili kuponya na kujenga upya maisha na jamii zao". Kuanzishwa kwake kulichochewa na mauaji ya halaiki ya Sinjar.[3]

Mnamo 2018, yeye na mtaalamu wa magonjwa ya wanawake wa Kongo Denis Mukwege walitunukiwa kwa pamoja Tuzo ya Amani ya Nobel kwa "juhudi zao za kukomesha matumizi ya ukatili wa kijinsia kama silaha ya vita na migogoro ya silaha ." [4] Yeye ndiye raia wa kwanza wa Iraqi na Yazidi kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel.

Mnamo mwaka 2016, Murad aliteuliwa kuwa Balozi wa Nia Njema wa kwanza kabisa wa Heshima ya Wanusurika wa Usafirishaji Haramu wa Binadamu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu [5]

  1. "Nobel Peace Prize awarded to Denis Mukwege and Nadia Murad". Deutsche Welle. 5 Oktoba 2018. Iliwekwa mnamo 2 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Iraqi Yazidi human rights activist Nadia Murad gets married". Ekurd.net. 20 Agosti 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Januari 2019. Iliwekwa mnamo 23 Aprili 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Nadia Murad". Forbes. Iliwekwa mnamo 5 Oktoba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Announcement" (PDF). The Nobel Peace Prize. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 5 Oktoba 2018. Iliwekwa mnamo 5 Oktoba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Human trafficking survivor Nadia Murad named UNODC Goodwill Ambassador". United Nations. Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nadia Murad kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.