Nadabu wa Israeli
Mandhari

Nadabu wa Israeli (kwa Kiebrania נָדָב, Nāḏāḇ) alikuwa mwana wa Yeroboamu I akatawala kwa miaka 2 Ufalme wa Israeli[1][2] hadi alipouawa na kapteni wake Baasha ambaye alijifanya mfalme na kuangamiza familia yote ya Yeroboamu I kama alivyotabiri nabii Ahiya.
Biblia inamhukumu hasa kwa kuendeleza sera ya kidini iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi.
Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Kwanza cha Wafalme, 14-15.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nadav", Jewish Encyclopedia
- ↑ Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings, (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257
| Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nadabu wa Israeli kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |