Nabil Fekir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fekir akiwa mazoezini na timu ya taifa ya Ufaransa.

Nabil Fekir (alizaliwa 18 Julai 1993) ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji wa klabu ya Olympique Lyonnais.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Fekir alijiunga na chuo cha vijana wa Olympique Lyonnais akiwa na umri wa miaka 12, na miaka miwili baadaye aliachiliwa kwa kuwa hana nguvu.

Hapo alihamia Vaulx-en-Velin akaendelea na kazi yake ya ujana huko Saint-Priest, ambako alifuatiliwa na wapelelezi kutoka Ufaransa, Fekir alisaini mkataba wa miaka miwili na AS Saint-Étienne, lakini Lyon iliamua kumsajili tena mwaka 2011. Alisema "Nilitaka kuionyesha [Lyon] kwamba walifanya makosa".

Fekir alianza kuchezea timu ya taifa ya Ufaransa mwezi Machi 2015 na alichaguliwa katika kikosi cha Kombe la Dunia la 2018 ambapo aliisaidia timu yake kuchukua Kombe la Dunia 2018.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabil Fekir kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.