Nenda kwa yaliyomo

Nabii Hulda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaburi la Hulda.

Nabii Hulda (jina la Kiebrania: חֻלְדָּה, Ḥuldā; alizaliwa karne ya 7 KK) alikuwa nabii wa Israeli ya Kale ambaye habari zake zinapatikana katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 22:14-20 na katika Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 34:22-28.

Humo tunasoma kwamba, wakati wa mfalme Yosia, walipokuwa wanarekebisha na kutakasa hekalu la Yerusalemu, waliokota kitabu cha Sheria ya Mungu wakakipeleka kwa mfalme aliyeagiza kazi hizo, naye akatuma Hilkia, Ahikam, Akbor, Shafan na Asaia kwa Hulda ili kujua Bwana anataka wafanye nini. Hivyo mwanamke huyo akawa mtu wa kwanza kutambua maandishi kuwa Neno la Mungu[1].

Alikuwa mke wa stookipa Shallum bin Tokhath (au Tikvah) na alikuwa anaishi Yerusalemu[2].

  1. William E. Phipps, Assertive Biblical Women, p. 85.
  2. BibleGateway.com, Translations of 2 Chronicles 34:22

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabii Hulda kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.