Mwele Ntuli Malecela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mwele Ntuli Malecela
Tarehe ya kuzaliwa 26 Machi 1963
Chama CCM
Digrii anazoshika Shahada ya uzamivu
Kazi Mkurugenzi wa Taasisi ya tafiti za kiafya (NIMRI)


Mwele Ntuli Malecela (alizaliwa tarehe 26 Machi 1963) alikuwa mkurugenzi wa taasisi ya tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI) )[1] . Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.[2][3]Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela amekua akifanya kazi na shirika la chakula duniani (WHO) upande wa Africa kama msimamizi wa maswala ya utawala, sera na ushauri wa kidiplomasia.

Maisha ya awali na kazi[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuhitimu shahada ya kwanza katika masuala ya wanyama katika chuo kikuu cha Dar es Salaam[4] alijiunga na taasisi ya tafiti za kiafya (NIMRI) mnamo mwaka 1987. Katika kipindi hicho Mwele alifafanya tafiti za ugonjwa wa homa ya matende katika kituo cha Amani. Baadavya hapo aliendelea na elimu ya juu katika chuo kiitwacho London School of Hygiene and Tropical Medicine ambako alitunukiwa shahada yake ya pili mwaka 1990 na shahada ya uzamivu mwaka 1995. Aliendelea na tafiti zake katika taasisi ya NIMRI mpaka kufikia mwaka 1998 ambapo alipewa cheo cha mkurugenzi wa tafiti. Mwaka 2000 Mwele alikua kiongozi wa program ya homa ya matende, ambayo imekua ikifanya kazi katika wilaya takribani 53.

Maisha ya kisiasa[hariri | hariri chanzo]

Malecela alijiunga na chama cha Mapinduzi, CCM mnamo mwaka 1981 alipokua Kilakala. Kwa wakati huo alihitajika kupata mafunzo maalumu kwanza kabla ya kujiunga na chama cha mapinduzi. Dokta Malecela alifanya mafunzo hayo mwezi Aprili 1981[5] na baada ya hapo amekua mwanachama wa kudumu hadi kufikia sasa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]