Mwajuma Selemani Mohamed

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

mwajumaSelemani Mohamedi maarufu kama (Madam Nice) alizaliwa mwaka 1988 katika kijiji cha Jitengeni, Tarafa ya Mombo Wilaya ya Korogwe , Mkoani Tanga .

                ELIMU
Mwaka 1996-2002 alipata elimu ya msingi shule ya msingi Jitengeni. Mwaka 2003-2006 alipata elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Mazinde day. Mwaka 2008-2010 alipata elimu ya juu ya sekondari shule ya sekondari Mombo. Mwaka 2010 alichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma na kutunukiwa Shahada ya Ualimu katika saikolojia, huku somo lake la kufundishia likiwa ni kiswahili .

Mwaka 2014 aliajiriwa shule ya sekondari Macechu Jijini Tanga akifundisha somo la kiswahili.

HARAKATI ZAKE ZA UANDISHI. Mwajuma alianza kujishughulisha na uandishi wa Riwaya na Ushairi tangu alipokuwa anasoma sekondari. Kipaji hicho alikiendeleza hata alipokuwa Chuoni. Baada ya jitihada kubwa sana alizozionyesha chuoni kama mdau mkubwa wa kiswahili hatimae alijiunga na CHAMA CHA WANAFUNZI WA KISWAHILI VYUO VIKUU VYA AFRIKA YA MASHARIKI (CHAWAKAMA) na kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, na baade muweka hazina, katika kitivo cha Elimu Chuo Kikuu cha Dodoma. Mwandishi huyu hakuishia hapo katika kuipigania lugha hii adhimu ya kiswahili kwani aliamua kujiunga na CHALUFAKITA na mwaka 2017 alipata tuzo ya mwalimu mbunifu wa somo la kiswahili. Mpaka sasa ni mjumbe wa CHAMA CHA LUGHA NA FASIHI YA KISWAHILI TANZANIA (CHALUFAKITA) kanda ya kaskazini.

Mwaka 2018 mwezi wa 4 aliteuliwa kuwa mjumbe na kiongozi wa kanda ya kaskazini, katika utafiti uliofanywa na Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA) ambalo ni tawi la Jumuia ya Afrika Mashariki. 

Sio hivyo tu bali ni Mwenyekiti wa CHAWAVITA) Chama cha Waandishi wa Vitabu Tanzania . hadi sasa Mwajuma amefanikiwa kutoa kitabu kimoja kiitwacho NDOA YA USALITI Pamoja na kwamba hiki ndicho kitabu chake cha kwanza kukichapisha lakini mwandishi huyu anamiswada mingine ambayo yuko mbioni kuichapisha kama vile: