Muziki kwenye miaka ya 1990

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muziki maarufu
Ratiba ya matukio ya muziki
Orodha ya mitindo maarufu ya muziki

Muziki uliotamba sana katika miaka ya 1990 tuliona mwendelezo wa teen pop na dance-pop mitindo ambayo ilianzishwa katika miaka ya 1970 na 1980. Isitoshe, hip hop inakua na kuendelea kuwa na mafanikio makubwa sana katika muongo huu, ikiwa na mwendnelezo wa zama za dhahabu za muziki wa hip hop.

Mbali na kurap, muziki wa contemporary R&B na urban ulibaki kuwa maarufu mno katika muongo huu; muziki wa urban mwishoni mwa miaka ya 1980 na 1990 mara nyingi ulihusiana na na mitindo kama vile soul, funk na jazz, na kupelekea mitindo mingine kama vile new jack swing, neo-soul, hip hop soul na g-funk ambayo yote ilitamba sana.

Mitindo maarufu kwa 1990[hariri | hariri chanzo]

Adult Contemporary[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, vibao vikali vya Mariah Carey kama vile "Vision of Love" (1990), "Love Takes Time" (1990), kibao cha Whitney Houston "All the Man That I Need" (1990) na "I Will Always Love You" (1992) zilitamba sana katika chati za miondoko hii ya adult contemporary.[1]

Contemporary R&B[hariri | hariri chanzo]

Katika miaka ya 1990, kazi ya Mariah Carey ilitokana na quiet storm, ikiwa na vibao vikali kama vile "Vision of Love" (1990), na "Love Takes Time" (1990). Albamu yake ya Music Box na Daydream ni miongoni mwa albamu zilizouza vyema kwa muda wote, na zilikuwa na athira kubwa za R&B. Quiet storm ya Whitney Houston ni vibao vyake vikali kama vile "All the Man That I Need" (1990) na "I Will Always Love You" (1992).

Kibao cha Houston I Will Always Love You kilitumia majuma 14 kikiwa nafasi ya kwanza katika chati za Billboard Hot 100 kwa kipindi hicho, na kuuza nakala zaidi ya milioni 20 dunia nzima. Ni kibao pekee kilichouza vyema kwa msanii wa kike kwa muda wote. Tena mwanzoni mwa miaka ya 1990, Boyz II Men walivumisha tena muziki wa classic wenye mvuto-wa-soul. Michael Jackson alishiriki new jack swing katika albamu yake ya mwaka 1991 Dangerous, kwa kupiga mauzo zaidi ya milioni 50, na kuwa miongoni mwa albamu zilizouza vyema kwa muongo huu.[2][3]

Umaarufu wa ballad na R&B umepelekea kuanzishwa kwa mtindo uitwao Urban adult contemporary. Miongoni mwa wasanii maarufu wa R&B nchini Marekani ni pamoja na Mariah Carey, Faith Evans, D'Angelo, Lauryn Hill, Whitney Houston, Sade, En Vogue, Toni Braxton, Boyz II Men, Mary J. Blige, Dru Hill, Vanessa L. Williams, Groove Theory, Bell Biv Devoe, Jodeci, Diana King, Tony! T

Mariah Carey alitangazwa kuwa msanii wa Muongo wa 1990 na jarida la Billboard.

oni! Tone!, Tara Kemp, Brownstone, Shanice, Usher, SWV, Aaliyah, Keith Sweat, R. Kelly, TLC, Xscape, Brandy, Monica, na Tevin Campbell. Kwa kutofautisha na kazi za Boyz II Men, Babyface na wasanii wa namna hii wanaofanana, wasanii wengine wa R&B kutoka katika kipindi hiki walianza hata kuongeza zaidi midundo ya hip hop katika kazi zao.

Katikati mwa miaka ya 1990s, Janet Jackson, Mariah Carey,Faith Evans, TLC, Xscape, Whitney Houston na Boyz II Men waliileta contemporary R&B katika ramani.

Albamu ya Jackson yenye-jina-lake janet. (1993), ambayo imekuja baada ya mkataba wake wa malioni-ya-dola-kihistoria aliofanya na Virgin Records, imeuza zaidi ya nakala milioni kumi dunia nzima. Houston, Boyz II Men na Carey walirekodi vibao kadhaa vilivyoshika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100, ikiwa ni pamoja na "Exhale (Shoop Shoop)", "One Sweet Day", ushirikiano baina ya Boyz II Men na Carey, kibao ambacho kilitamba kwa muda mrefu kikiwa nafasi ya kwanza kwenye historia ya Hot 100, Boyz II Men na TLC wametoka albamu mnamo 1994 na 1995—Daydream, II, na CrazySexyCool – ambayo iliuza zaidi ya nakala milioni kumi, na kuwapatia hadhi ya almasi nchini Marekani mwanzoni mwa mwaka wa 1995, kina Grammy Awards wakaanzisha Grammy Award for Best R&B Album, ikiwa II (Boyz II Men) Boyz II Men wanakuwa kama kundi la kwanza kupokea tuzo hiyo. Tuzo hiyo baadaye ilienda pia kwa TLC kwa ajili ya albamu yao ya CrazySexyCool ya mwaka wa 1996.

Wimbo ulioimbwa pamoja kati ya Mariah Carey na Boyz II Men "One Sweet Day" ulitangazwa kama wimbo bora wa muongo, ulishika namba moja katika chati za mwishoni-mwa-muongo. Carey akawa msanii wa kike wa Billboard mwenye mafanikio zaidi kwa muongo, na mmoja kati ya wasanii wa R&B mwenye mafanikio makubwa sana kwa miaka ya 90.

Wasanii wa R&B kama vile Janet Jackson, Michael Jackson, Whitey Houston na Mariah Carey ni miongoni mwa wasanii waliouza vyema kwa muda wote, na hasa katika miaka ya 1990 waliileta Contemporary R&B katika jukwaa la ulimwengu.

Hip hop[hariri | hariri chanzo]

Lauryn Hill alikuwa miongoni mwa wasanii wa muziki wa hip hop wa kike wenye mafanikio makubwa sana kwa miaka ya 1990.
Jay-Z akawa miongoni mwa wasanii wa hip hop wenye mafanikio makubwa kunako miaka ya 1990.

Albamu ya Dr. Dre ya mwaka wa 1992 The Chronic ilitoa mwongozo mkuu wa gangsta rap.[4] Kufuatia mafanikio makubwa waliyopata Death Row Records, West Coast hip hop ilitingisha sana hip hop mwanzoni mwa miaka ya 1990, pamoja na The Notorious B.I.G. kwa upande wa East Coast.[5] Hip hop ikawa moja kati ya mtindo uliofanya mauzo bab-kubwa ilivyofika katikati mwa miaka ya 1990.[6][7]

Mwaka wa 1998, Lauryn Hill ametoa albamu yake ya kwanza The Miseducation of Lauryn Hill, ambayo iliingia moja kwa moja hadi nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200. Mwaka wa 1999, The Miseducation ilipata kuchaguliwa mara 10 katikaa tuzo za Grammy, imeshinda tano (ambapo kwa kipindi hicho haijawahi kusikika kwa msanii wa hip-hop) na hatimaye imeenda kuuza nakala miliono 19 kwa hesabu ya dunia nzima.[8]

Ile miaka ya mwanzoni mwa 1990 ilitawaliwa na marapa wa kike, kama vile Queen Latifah na kundi la muziki wa hip hop linaloendeshwa na wasanii watatu Salt-n-Pepa. Mwishoni mwa miaka ya 1990 tumeona kuibuka kwa marapa wengi wa kike walioingia huko East Coast hip hop, kukiwa na kutolewa kwa albamu ya kwanza ya Lil' Kim (na Hard Core) na Foxy Brown (na albamu yake ya Ill Na Na), hasa kwa kuzidi kwao kujionesha maungo yao na mistari yenye miropoko ya haja.

Mwishoni mwa miaka ya 1990 kibao kimegeukia upande wa dirty south na crunk, kukiwa na wasanii kama vile Outkast, Ludacris, Jay-Z, Missy Elliott na Lil Wayne.[9]

Katikati mwa miaka ya 90 kulijulikana sana kwa vifo vya marapa wa West Coast, 2Pac, na East Coast, The Notorious B.I.G., ambao wanadaiwa kuuawa na kupelekea Uhasimu wa hip hop ya East Coast–West Coast.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ripani, Richard J. (2006), The New Blue Music: Changes in Rhythm & Blues, 1950–1999, Univ. Press of Mississippi, pp. 130–155, 186–188, ISBN 1-57806-862-2 
  2. "Michael Jackson sulla sedia a rotelle", AffarItaliani.it, 11 July 2008. Retrieved on 10 May 2009. Archived from the original on 2009-04-16. 
  3. Carter, Kelley L.. "New jack swing", Chicago Tribune, 11 August 2008. Retrieved on 21 August 2008. Archived from the original on 2008-12-16. 
  4. "The missing link of hip-hop's golden age", The Guardian, 3 January 2008. Retrieved on 17 September 2011. 
  5. "MYTH No. 4: Biggie & Tupac Are Hip-Hop's Pillars", SPIN, 9 November 2009. Retrieved on 4 September 2011. Archived from the original on 2013-12-07. 
  6. "The hip-hop heritage society", The Guardian, 7 October 2010. Retrieved on 8 November 2011. 
  7. "The music dies for once popular 'Guitar Hero' video game", CNN, 9 February 2011. Retrieved on 27 November 2011. Archived from the original on 2011-08-11. 
  8. Rolling Stone article: "Inside "The Miseducation of Lauryn Hill: page 1 Archived 27 Aprili 2009 at the Wayback Machine.."
  9. "Simon Reynolds's Notes on the noughties: When will hip-hop hurry up and die?", The Guardian, 26 November 2009. Retrieved on 25 August 2011. 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]