Muungo metali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muungo au mbabadi metali hupatikana katika metali kama kupri kutokana na kani kati ya elektroni huria yenye chaji ya hasi na viini vya atomi vyenye chaji ya chanja.

Muungo metali (pia: mbabadi metali, en:metallic bonding) ni jinsi atomi za metali zinavyoshikana. Kani hii yatokana na elektroni huria zinazotembea kati ya atomi na kuvutwa na ioni za kiini.

Kwa metali elektroni za mzingo elektroni wa nje hazishikwi sana na kiini, hivyo ni rahisi kuachana na atomi asilia na kuzunguka katika metali yote. Viini vya atomi vyenye chaji chanya vinajipanga katika mfumo maalumu unaofanana na fuwele. Elektroni zinazunguka katika mfumo huo kama wingu.

Hali hiyo ya kuwa na elektroni huria yaeleza tabia za metali kama vile kuwa wayaikaji, kung'aa na kupitisha joto na umeme kwa urahisi. Elektroni huria zinapitisha nishati kama joto au umeme haraka na wepesi ndani ya metali - tofauti na dutu ambamo kila elektroni yashikwa imara katika atomi yake.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muungo metali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.