Nenda kwa yaliyomo

Muungano wa Wafanyakazi wa Viwanda vya nguo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Muungano wa wafanyakazi wa viwanda vya nguo ulikuwa chama cha wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi katika viwanda vya nguo nchini Afrika Kusini.

Muungano huo ulianzishwa mwaka 1935 na uliunganishwa na Baraza la Vyama vya wafanyakazi na Kazi la Afrika Kusini. Kilikuwa kitu cha pekee kwa sababu kilikubali wanachama weusi na weupe na katika maeneo ya Cape town na Harrismith yalikua sehemu ya matawi yaleyale.Nafasi hii iliongozwa na Katibu Mkuu wa muungano Roy du Preez. Mwaka 1942 ulisaidia kupanga upya muungano wa wafanyakazi wa kufua nguo wa Kiafrika. Mwaka 1950 muungano ulipigwa marufuku kuwakilisha wafanyakazi weusi na weupe kwa pamoja. Hivyo bhasi ukaundwa Muungano wa wafanyakazi wa nguo za Kiafrika kuwakilisha wafanyakazi weusi. Mwaka 1954 wanachama weupe walijitenga na kuanzisha muungano wao wa kibaguzi.

Muungano uliobakia uliendelea kushirikiana na baraza la Vyama vya Wafanyakazi Afrika Kusini. Mwaka 1987 uliungana na Muungano wa kitaifa wa Wafanyakazi wa nguo na Muungano wa Kitaifa wa Wafanyakazi wa Mavazi na kuunda Muungano wa pamoja na wafanyakazi wa mavazi na nguo wa Afrika Kusini.