Music of Zimbabwe
Muziki wa Zimbabwe unategemea sana matumizi ya vyombo vya asili kama mbira, ngoma na hosho. Muziki huu una maana kubwa zaidi ya kuwa burudani tu, kwani aina za muziki wa asili na wa kisasa zilitumika kama ishara ya matumaini kwa Wazimbabwe waliokuwa wakipigania uhuru kutoka utawala wa Rhodesia.
Muziki umekuwa na nafasi muhimu katika historia ya Zimbabwe. Umetumika katika sherehe za jadi za Bira kwa ajili ya kuwaunganisha watu na kuomba msaada wa roho za mababu, na pia ulitumika kama njia ya kutoa ujumbe wa kupinga ukandamizaji wakati wa harakati za kupigania uhuru.
Jamii ya Zimbabwe ilitumia muziki kueleza malalamiko yao na kupinga mateso waliyokuwa wakipitia, kwa kuwa ulikuwa mojawapo ya njia muhimu walizoweza kutumia kutoa sauti yao.
Katika miaka ya 1980, muziki wa Zimbabwe ulikuwa maarufu sana katika eneo la Afrika kutokana na aina za muziki kama Sungura na Jit. Hata hivyo, baadhi ya wanamuziki walizuiwa kuonekana kwenye televisheni na redio za serikali, hali iliyosababisha baadhi ya maeneo ya burudani kufungwa.[1][2][3] [4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]{{reflist}}
| Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Music of Zimbabwe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ Dwamena, Anakwa. "Zimbabwe's Powerful Music of Struggle". The New Yorker (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-11-30.
- ↑ Popoola, Tayo. "True Jit Bulawayo". BBC. Iliwekwa mnamo 2021-04-07.
- ↑ "An eviction that inspired the "Evicted Band"". Business Times. 20 Julai 2018. Iliwekwa mnamo Julai 20, 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Zimbabwe's Dividing The Element Unleash The World's First Shona Metal Album". Rock Pit. Mei 23, 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)