Nenda kwa yaliyomo

Musa Qazimi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Musa Qazimi (1864 – 7 Julai 1915) alikuwa mwanasiasa na mwasi wa Albania.[1] Akiwa Turkophilia na Mufti aliyependa utamaduni wa Uturuki, kwanza alikuwa meya (1904–1908), kisha akawa mufti (1908–1913), na mwishowe mkuu wa mkoa (prefect) wa Tirana (1913–1914). Katika kipindi cha misukosuko baada ya Azimio la Uhuru wa Albania kutoka kwa Dola la Osmani, kwanza alikuwa muungaji mkono wa kundi la Waturuki Vijana (Young Turks), na baadaye wa Essad Pasha.

Baada ya kutofautiana na Essad Pasha, aliasi na kuwa kiongozi katika Uasi wa Wakulima nchini Albania na uasi wa kijimbo, wa kurejesha mifumo ya kale]] na uliojaa misingi ya kidini wa kuunga mkono utawala wa Ottoman dhidi ya mamlaka mpya ya serikali ya Albania. Ingawa kiongozi mkuu rasmi wa harakati hiyo alikuwa Haxhi Qamili na kiongozi wa majeshi yake alikuwa Mustafa Ndroqi, Qazimi amekuwa akichukuliwa kama kichocheo cha kiitikadi cha harakati hiyo,[1] na "kiongozi halisi" wa uasi huo.[2]

Baada ya uasi huo kusambaratishwa na muungano wa dharura ulioundwa na Wakatoliki wa kabila la Mirdita, wapiganaji wa kizawa, Waalbania wa Kosovo wakiongozwa na Isa Boletini, na baadhi ya watu wa kujitolea kutoka nje hasa kutoka Romania, alipatikana na hatia ya kupanga mauaji yaliyotokea wakati wa uasi wake dhidi ya waungaji mkono wa harakati ya kitaifa ya Albania pamoja na Wabektashi na Wakristo, na alinyongwa tarehe 7 Julai 1915.

  1. 1 2 Kristo Frashëri (2008). Historia e qytetërimit shqiptar: nga kohet e lashta deri ne fund të Luftës së Dytë Botërore. Akademia e Shkencave e Shqipërisë. uk. 245.
  2. Abas Ermenji (Januari 14, 2018). "LEVIZJA DUMBABISTE (TURKOMANE) E MUSA QAZIMI, LEVIZJE ANTISHQIPTARE (1914)". Vendi që zë Skënderbeu në historinë e Shqipërisë. Çabej. uk. 369. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 12, 2018. Iliwekwa mnamo Agosti 11, 2018.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Musa Qazimi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.