Nenda kwa yaliyomo

Murray River

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mto Murray (Murray River)
Murray kule Nyah, Victoria
Chanzo Snowy Mountains
Mdomo Goolwa, South Australia
Nchi Australia
Urefu km 2,575
Kimo cha chanzo m 1,430
Tawimito upande wa kulia Swampy Plains River, Murrumbidgee River, Darling River
Tawimito upande wa kushoto Mitta Mitta River, Kiewa River, Ovens River, Goulburn River, Campaspe River, Loddon River
Mkondo m3 767
Eneo la beseni km² 1,061,469
Murray ni mto mrefu kabisa wa Australia
Mto Murray katika milima huko Tom Groggin

Mto Murray ndio mto mrefu kabisa kwenye bara la Australia. Huanza kwenye Snowy Mountains na hutiririka magharibi hadi kuishia kwenye Bahari Pasifiki karibu na Goolwa, Australia Kusini.

Kwa sehemu kubwa ya njia yake huwa mpaka kati ya majimbo ya Victoria na New South Wales . Matawimto yanayojiunga na Murray ni pamoja na Mto Darling, Mto Lachlan, Mto Murrumbidgee na Mto Goulburn.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kwa maelfu ya miaka, Mto Murray umejulikana kwa Waaustralia asilia waliouita kwa majina yao kama vile Millewa na Tongala.

Mto huo uliitwa Mto wa Hume baada ya kutembelewa na wapelelezi wa Ulaya Hamilton Hume na William Hovell mnamo Novemba 1824. Baadaye lilibadilishwa kwa kuita mto kwa jina la mwanasiasa Mwingereza, Sir George Murray.

Usafiri kwenye mto ulikuwa na ugumu mwanzoni kwa sababu mdomo wa Murray baharini haina kina ya kutosha kwa meli kuingia mtoni. Tangu mwaka 1853 meli ndogo zilipelekwa barani zikaanzisha usafiri wa mtoni. [1]

Mto ulikuwa muhimu sana kwa kubeba watu na bidhaa hadi kujengwa kwa reli. Kufikia mwaka 1900 biashara ya mtoni ilikuwa imekwisha tena. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "The River Murray". South Australian History. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-07-20. Iliwekwa mnamo 2008-08-13.
  2. Australian Encyclopaedia Vol. VI. Angus and Robertson. 1958. ku. pg 208. {{cite book}}: |pages= has extra text (help); Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya audio na video[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Australia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Murray River kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.