Muhammad Kazim Khurasani
Mandhari
Muhammad Kazim Khurasani (1839 – 12 Desemba 1911), anajulikana zaidi kama Akhund Khurasani [1][2][3] alikuwa mwanasheria wa Kiislamu wa dhehebu la Shia na mwanaharakati wa kisiasa.[4]
Anajulikana kwa kutumia nafasi yake kama Marja' ili kuhalalisha na kuunga mkono mapinduzi ya kwanza ya kidemokrasia barani Asia yaliyotokea nchini Iran (1905–1911), ambapo yeye alikuwa mhimili mkuu kutoka upande wa viongozi wa kidini walioasisi mapinduzi hayo. Aliamini kuwa mfumo wa serikali ya kidemokrasia ungekuwa chaguo bora zaidi linalowezekana wakati huu ambao Maimamu Kumi na Wawili hawapo, na aliyachukulia mapinduzi ya kikatiba ya kidemokrasia kama Jihad (vita vitakatifu) ambavyo kila Mwislamu alipaswa kushiriki.[5][6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Farzaneh 2015, pp. 119–190.
- ↑ Hermann 2013, pp. 430–453.
- ↑ Hairi, A.; Murata, S. (1984). "AḴŪND ḴORĀSĀNĪ". Encyclopædia Irannica.
- ↑ Farzaneh 2015, p. 153.
- ↑ Hermann 2013, pp. 431, 435.
- ↑ Farzaneh 2015, pp. 159–162.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muhammad Kazim Khurasani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |