Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Wash 255 initiative

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

WASH 255 INITIATIVE

UCHAMBUZI

Tunapenda kuipongeza serikali katika jitihada kubwa inazofanya ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za maji safi na salama pamoja na usafi wa mazingira. Vilevile tunatambua mchango wa taasisi zizizo za serikali katika kufanikisha miradi ya maendeleo ya maji na usafi wa mazingira.

Katika hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya maji na umwagiliaji ya 2016/2017 iliyotolewa na waziri wa maji na umwagiliaji Mh.injinia Gerson Hosea Lwenge alidhihirisha kwamba takwimu za kimataifa zinzonyesha kua hatua madhubuti zisipochukuliwa ifikapo mwaka 2035 kiwango cha maji kilichopo kinaweza kupungua huku akitaja mabadiliko ya tabia nchi ni moja ya sababu na changamoto kubwa inayoikumba wizara.

Aidha alianisha changamoto nyingine zinazoikumba wizara kama madeni makubwa ya taasisi na makandarasi; ushiriki hafifu na sekta binafsi; uendelevu wa maji; na upungufu wa wataalamu.

Waziri alieleza juu ya uondoaji wa maji taka ambapo alikili kua huduma za uondoaji maji taka ni ndogo ambapo ni 20% kwenye miji yenye mitandao kama Dar es salaam,Arusha, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Mwanza ,Tabora, Moshi ,Tanga ,Songea na Iringa.

Pia katika hotuba hio alielezea jukumu la wizara la kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji ambapo wizara imejikita katika udhibiti kwenye mabonde ya wami/ruvu, Rufiji, ziwa Victoria, ziwa nyasa na bonde la ziwa Rukwa. Waziri alitaja moja ya sababu ya migogoro katika matumizi ya maji kwenye maeneo ya vyanzo vya maji ni wananchi kutokujua sheria na kanuni za matumizi bora ya maji.

MAPUNGUFU 1.Wizara imeonyesha ushiriki mdogo katika usafi wa mazingira huku wananchi wengi wakikosa huduma bora za vyoo na kuishi katika mazingira hatarishi kotokana na elimu ndogo na kukosa mwongozo mzuri wa serikali

2. Wizara haija ainisha udhibiti wa utiririshaji wa kemikali na maji taka katika vyanzo vingine vya maji kama mito midogo midogo inayotumiwa na wananchi wengi kwa shughuli mbalimbali.

3.elimu juu ya matumizi bora ya maji pamoja sheria ya maji na usafi wa mazingira namba 12 ya mwaka 2009 bado wananchi wengi hawazifahamu.

》Takwimu za shirika lisilo la kiserikali la WaterAid zinaonyesha 44% ya watanzani hawapati huduma za maji safi amapo Tanzania ni nchi ya tisa kati ya kumi duniani zenye watu wanaoishi bila huduma zamaji safi.

Vilevile ni nchi ya saba kati ya kumi duniani zenye idadi kubwa ya watu wanaoishi bila huduma za maji safi takribani watu million ishirini na tatu (23,239,992) hawapati huduma za maji safi.

Wanawake na watoto hutumia masaa mawili kwa siku kutafta maji na hadi masaa saba katika maeneo ya pembezoni. Upatikanaji wa vyoo ni mdogo ambapo 15% ya watanzania wote ndo hupata huduma hio. Hii imepelekea matatizo makubwa katika afya ambapo watoto 4000 chini ya umri wa miaka mitano wanafariki kila mwaka kwa magonjwa yanayozuilika ya kuharisha kutokana na huduma duni za maji na usafi wa mazingira.

Katika ripoti iliyotolewa na ESAWAS (Eastern and southern Africa water and sanitation) ambayo ni taasisi ya udhibiti inayojumuisha mamlaka kubwa za maji na usafi wa mazingira za Lusaka Zambia, Maputo Mozambique,Nairobi Kenya,Dar es salaam Tanzania, Lesotho na Rwanda inaonyesha DAWASCO inautendajiusio na uwiano wenye utendaji mkubwa kwenye kipengele cha ufanisi wa uchumi, utendaji wa kati katika kipengele cha uendelevu wa miradi na utendaji wa chini katika kipengele cha ubora wa huduma wanazotoa.

Bado Dar es Salaam imekua na miundo mbinu mibovu ya maji taka na maji safi na wananchi wengi huishi katika mazingira yenye huduma duni za maji na usafi wa mazingira na kupelekea milipuko ya magonja kama ya kipindupindu kila mara.

MAPENDEKEZO

>Serikali iweke kipaumbele katika usafi wa mazingira, kutoa elimu kwa wananchi, kuimarisha huduma za maji taka na kuongeza udhibiti wa utiririshaji wa maji taka na kemikali katika vyanzo vyote vya maji

 >Elimu juu ya mabadiliko ya tabia nchi lazima iongezwe na serikali iweke juhudi nyingi katika kumudu rasilimali za maji na kuziimarisha ili kupelekea uhifadhi wa maji

 >Serikali iwe na mipango iliopo kwenye mtiririko ikihusisha mipango miji ili kuepusha upotevu wa fedha zinazotumika katika miradi mbalimbali maji kuharibiwa na miradi mingine mfano barabara

 >Kuongeza ushirikishwaji wa wananchi na kuweka vipaumbele katika mipango ya maendeleo endelevu kwani hutegemeana sana