Mtumiaji:Waénwa Asumani
Wa'énwa Ethnic Books
[hariri | hariri chanzo]Wa'énwa Asumani Jay, Mwandishi wa Kibembe
Karibu
[hariri | hariri chanzo]Je, wewe ni Mbembe, rafiki, jirani, mume ama mke? Hapa umefika mahali husika kabisa!
Unajua, toka zamani za mababu, Mbembe hakuandika! Hiyo ilisababisha giza kubwa sana katika kizazi cha sasa, kuyajua mambo ya zamani. Sasa ni wakati wa kufanya nguvu kuandaa kizazi cha sasa, ili kizazi kinachokuja kesho, kisipotee kuliko sisi. Nawashukuru sana vijana na wazee wa Kibembe ambao wanajitahidi kuandika japo mammbo madogo ya ukoo wa Mbembe, Mbarikiwe sana! Tunajua sote kwamba kuanzia miaka ya 1950, Mbembe alianza kuandika, lakini aliandika mambo ya kanisa la Kristo pekee na kuacha mambo mengine muhimu maishani kama mila na desturi, malezi ya watoto, lugha, historia nk... Hiyo ni kwa vile kazi hiyo ilipata ushawishi mkubwa wa kanisa la Methodist na askofu wake Akúlú Ilangi akawa mmoja wa Waandishi wa zamani wa Kibembe. Abekya Mwalé naye akaandika kitabu cha Marko ndani ya Agano jipya. Kanisa likawasaidia kutoa tafsiri ya Biblia nzima baadaye. Lakini juhudi zao hizo zikawa na msaada mdogo kwa jamii ya Kibembe kwa vile zilisaidia Wakristo peke yao na siyo jamii nzima. Huu ni wakati sasa wa Wabembe wote kusimamia kazi hii mpaka ufanyikiwe kwa jinsi vijana na wazee, wote wamejitoa kuandika. Halafu pia, usisahau kwamba, Mbembe anatangazwa tofauti na vile alivyo katika dunia nzima. Tafadhali, tusaidiane kupanua kazi hii ili isaidie watoto wetu, wajukuu, vitukuu na vizazi vingine vinavyo kuja nzuma waishi kwa amani na umoja pia mshikamano. Naamini kama umesoma ukurasa wangu huu, hautakosa la kufanya kwa ajili ya jamii yako ya watoto wa Mbembe III M'mém'wa. Asante sana na Mungu wetu Abeca Púngú, akubariki sana.